Vladimir Putin: " Tumefikia mkutano wa amani kuhusu Ukraine"
...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/vladimir-putin-tumefikia-mkutano-wa.html
Kutoka
kushoto kwenda kulia, rais wa Belarusi, Alexander Lukashenko na viongzi
wanne Vladimir Putin, Angela Merkel, François Hollande na Petro
Poroshenko, Jumatano Februari 11 mwaka 2015
Na RFI
Rais wa
Urusi, Vladimir Putin amehakikishia vyombo vya habari baada ya mkutano
wa amani mjini Minsk, kwamba wamefikia mkataba wa amani kuhusu Ukraine.
Vladimir
putin, amebaini kwamba mkutano huo unahusu masuala mawili nyeti:
usitishwaji mapigano kuanzia Februari 15, pamoja na kuondoa silaha za
kivita mashariki mwa Ukraine.
"
Tumefanikiwa kufikia mkataba kuhusu masuala nyeti", amesema rais wa
Urusi katika mkutano wa amani kuhusu Ukraine unaofanyika katika mji mkuu
wa Belarusi, Minsk. Viongozi wa Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Ukraine
wanakutana tangu Jumatano wiki hii mjini Minsk, kujaribu kutafutia
suluhu machafuko yanayoendelea Ukraine.(P.T)
Hayo
yanajiri wakati mapigano kati ya jeshi la ukraine na waasi wanaotaka
kujitenga kwa eneo la mashariki yanaendelea kushika kasi kila kukicha.
Mtu mmoj aliuawa Jumatano katika mashambulizi karibu na hospitali ya
mjini Donetsk.
Duru
kutoka Ukraine zilikua zinafahamisha kwamba viongozi katika mkutano huo
Jumatano usiku wiki hii walikua wanatazamiwa kutia saini katika tangazo
la pamoja ya kuunga mkono uhuru wa Ukraine.
Rais
Alexandre Loukachenko, ambae anachukuliwa kama dikteta barani Ulaya,
amewapokea viongozi wa Urusi na Ukraine, na vile vile François Hollande
na Angela Merkel. Ni kwa mara ya kwanza tangu miaka 76 iliyopita,
kiongozi katika ngazi ya juu nchini Ujerumani kuingia katika mji wa
Minsk, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu katika utawala wa Georges
Pompidou mwaka 1973, rais wa Ufaransa akijielekeza katika mji huo wa
Minsk.
Rais wa
Ufaransa, François Hollande, amesema juhudi za kidiplomasia zinaendelea
kuzuia Ukraine kutumbukia katika dimbwi la machafuko.
Kwa
mujibu wa mwandishi wa RFI Minsk, Muriel Pomponne, Jumatano jioni wiki
hii, baada ya saa moja na nusu ya mkutano, mazungumzo yaliendelea kwa
upana yakiwajumuisha wajumbe mbalimbali kutoka mataifa hayo
yanayochangia ili amani ya kudumu ipatikane nchini Ukraine. Viongozi hao
wanne pamoja na washauri wao walikua wakijadili stakabadhi
ziliyoandaliwa kwa siku kadha na wanadiplomasia wao.
Hayo
yakijiri, watu 47 waliuawa katika mapigano yaliyotokea Jumanne wiki hii.
Rais wa Ukraine ametishia kuwa iwapo mazungumzo hayo yataambulia
patupu, sheria ya kijeshi itatekelezwa katika nchi nzima ya Ukraine.