Flatnews

Serikali kusambaza nakala milioni mbili za katiba inayopendekezwa

Marais Dkt. Jakaya Kikwete na Dkt Ali Shein mara baada ya kukabidhiwa Katiba inayope...




Marais Dkt. Jakaya Kikwete na Dkt Ali Shein mara baada ya kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa.
Marais Dkt. Jakaya Kikwete na Dkt Ali Shein mara baada ya kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa.
Waziri Migiro akiongea na baadhi ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Migiro akiongea na baadhi ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Dar es salaam, Serikali imeanza mchakato wa  kusambaza nakala milioni mbili za Katiba Inayopendekezwa nchini kote.  Hatua  itakayowawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni.
Kwa mujibu wa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro amesema leo kuwa kati ya nakala hizo zimechapwa jijini Dar es Salaam ambapo  nakala 1,800,000 zinasambazwa Tanzania bara na nakala 200,000 zinasambazwa Tanzania Zanzibar.
Ameongeza kuwa  hadi kufikia jana (Jumanne, Februari 10, 2015), jumla ya nakala 707,140 zilikuwa zimesambazwa katika mikoa 12 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambayo imepata nakala 200,000 na kuwa kazi hiyo inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao.
Mikoa hiyo na nakala ziliozosambazwa  ni Katavi (15,640), Rukwa (27,040), Ruvuma (47,740), Mbeya (78,640), Simiyu (34,840), Mara (52,540), Tabora (58,540) na Kigoma (41,440). Mikoa mingine ni Kagera (54,340), Geita (36,940), Mwanza (57,040) na Pwani ambapo usambazaji umeanza kwa wilaya ya Mafia ambayo imepata nakala 2,400.
“Idadi ya nakala ya Katiba Inayopendekezwa kwa kila mkoa inategemea na wingi wa kata katika mkoa, ndiyo maana baadhi ya mikoa unaona imepata nakala nyingi,” amesema Dkt. Migiro ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya waandishi wa Habari waliotaka ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa katika kazi ya uchapishaji na uasambazaji wa nakala za Katiba Inayopendekezwa.
Zaidi kata 3,800 nchini kote zinatarajia kupata nakala hizo  na lengo la Serikali ni kusambaza nakala 300 katika kila kata ambazo zitasambazwa kwenye vijiji, vitongoji na mitaa kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji.
Kwa upande wa  taasisi za elimu na dini, Waziri Migiro amesema Serikali imepanga kusambaza nakala 658,400 kwa taasisi za elimu, dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia na kuwa usambazaji huo utaanza hivi karibuni.
Katika hatua nyingine  amewakumbusha wananchi ambao bado hawajapata nakala za Katiba inayopendekezwa, kuisoma kupitia tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria (www.sheria.go.tz).

Related

PHOTOS 2515144931962922660

Post a Comment

emo-but-icon

item