ADAM LALLANA AKUMBANA NA 'ZOMEA-ZOMEA'
Adam Lallana (kushoto) alizomewa na mashabiki MENEJA wa Liverpool, Brendan Rodgers amekiri kushangazwa na jinsi nahodha wa ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/adam-lallana-akumbana-na-zomea-zomea.html
Adam Lallana (kushoto) alizomewa na mashabiki
MENEJA
wa Liverpool, Brendan Rodgers amekiri kushangazwa na jinsi nahodha wa
zamani wa Southampton, Adam Lallana alivyopokelewa vibaya akirejea
katika dimba la St Mary kwenye mechi ya ligi ambayo Liverpool
walishinda 2-0 jana.
Kiungo
huyo aliyekaa Southampton kwa miaka 14, alijiunga na Liverpool majira
ya kiangazi mwaka jana na jana alizomewa na mashabiki wa nyumbani kama
ilivyokuwa pia kwa Dejan Lovren aliyeondoka klabuni hapo kujiunga
Anfield mwishoni mwa msimu uliopita.
Mshambuliaji Rickie Lambert ambaye alikuwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba, ingawa hakucheza, yeye alipokelewa vizuri.
