Ongwen akabidhiwa kwa wanajeshi wa UG
Kamanda Ongwen sasa yuko mikononi mwa wanajeshi wa Uganda ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/ongwen-akabidhiwa-kwa-wanajeshi-wa-ug.html
Kamanda mkuu wa kundi la waasi la LRA nchini Uganda, aliyejisalimisha wiki jana, Dominic Ongwen , amekabidhiwa kwa wanajeshi wa Uganda walio katika Jamuhuri ya Afrika ya kati.
Waasi hao walisema kwamba walimkatama Ongwen baada ya makabiliano ya muda ingawa jeshi la Marekani lilisitiza kuwa alijisalimisha na tangu hao wamekuwa wakimzuilia.
Kundi la LRA liliwateka nyara wasichana na wavulana huku wavulana wakilazimishwa kuwa wapiganaji na wasichana wakifanywa watumwa wa ngono.
Ongwen pamoja na Joseph Kony wanatakikana na mahakama ya ICC kujibu tuhuma za kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Je Ongwen ni nani?
-Inaarifiwa alitekwa nyara na waasi wa LRA akiwa na umri wa miaka 10 wakati alipokuwa anaelekea shuleni Kaskazini mwa Uganda.
-Miaka iliyofuata, alipanda ngazi na kuwa kamanda
-Anatuhumiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo, kuwatumia watoto kama watumwa.
-ICC ilitoa kibali cha kumkamata mnamo mwaka 2005.
-Kuliwa na madai kwamba aliuawa katika mwaka 2013 ambapo Marekani ilitangaza ahadi ya zawadi kwa yeyeote mwenye taarifa kumhusu.