Mrisho Ngassa ajisalimisha Yanga
LICHA ya mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, kuwapigia simu viongozi wake juzi Jumanne, lakini wameahi...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/mrisho-ngassa-ajisalimisha-yanga.html
LICHA ya
mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, kuwapigia simu viongozi wake juzi
Jumanne, lakini wameahidi kuendelea kumchunguza kwa kuhusishwa na
kutimkia nchini Afrika Kusini
kwenda kufanya majaribio ya soka la
kulipwa, tofauti na alivyoomba ruhusa ya kushugulikia matatizo ya
familia yake.
Wiki
iliyopita Katibu wa Yanga, Jonas Tiboroha alikaririwa na Mwanaspoti kuwa
alisikia Ngassa ametimkia Afrika Kusini na alipojaribu kumtafuta kwenye
simu yake hakupatikana.(P.T)
"Nimepigiwa
simu na Ngassa usiku wa juzi Jumanne , tumezungumza mambo mbalimbali
ikiwemo kumuuliza maendeleo ya matatizo ya familia yake, lakini hilo
halinifanyi niache kuendelea kuchunguza ukweli juu ya tuhuma
zinazoelekezwa kwake," alisema.
Tiboroha
alisema endapo kama itabainika mchezaji wao kafanya kosa hilo
atawajibishwa ili iwe mfano kwa wachezaji wengine kuzingatia nidhamu ya
kazi zao za kufuata utaratibu unaotakiwa na siyo kufanya mambo kiholela.
Chanzo:Mwanaspoti