ESCROW YAWAFIKISHA WATATU KIZIMBANI
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/escrow-yawafikisha-watatu-kizimbani.html
MZIMU wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, limeendelea kuwatafuna
watuhumiwa wa uchotwaji wa mabilioni ya fedha za akaunti hiyo baada ya
watuhumiwa wengine watatu kupandishwa kizimbani katika mahakama ya
Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Waliopandishwa ni Meneja wa Misamaha ya Kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Leonard Mutabingwa ambaye anadaiwa kupokea rushwa ya
zaidi ya shilingi bilioni moja kama zawadi kutoka kwa Rugemalira,
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Mkombozi , Julius Ruta, ambaye anadaiwa
kupokea zaidi ya shilingi milioni 100 pamoja na Ofisa Mwandamizi wa
Tanesco, Steven Urasa, anayetuhumiwa kupokea zaidi ya shilingi
milioni 100.
Mpaka GPL inatoka mahakamani hapo ni mtuhumiwa mmoja tu aliyefanikiwa
kuwa nje kwa dhamana ya kuweka nusu ya fedha anazotuhumiwa kupokea
akitakiwa kuwa na watu wawili kama wadhamini. Watuhumiwa wengine
walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi zao kutajwa tena
tarehe 27, 29 Januari na 11 Februari mwaka huu.