Chelsea, Man City hakuna mbabe
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia goli lao Mechi kati ya Chelsea na Man...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/chelsea-man-city-hakuna-mbabe.html
Mechi kati ya Chelsea na Manchester City imemalizika kwa wababe hao wa Ligi Kuu ya Uingereza kufungana 1-1 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Stamford Bridge Jumamosi usiku.
Loic Remy aliipatia Chelsea goli la kuongoza dakika ya 42 lakini goli hilo halikudumu baada ya David Silva kuisawazishia timu yake dakika ya 45 na kuzifanya timu hizo zigawane point.
Chelsea bado wapo kileleni mwa ligi kwa pointi zao 53 huku Man City ikibaki nafasi ya pili baada ya kujikusanyia point 48.
