BREAKING NEWS: AJALI YAUA WATATU USIKU HUU ...NI BAADA YA KUGONGANA LORI NA BODA BODA NA kuteketea kwa moto-IRINGA
Saturday, January 31, 2015 Hizi ndivyo lori hilo lilivyoharibika
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/breaking-news-ajali-yaua-watatu-usiku.html
Saturday, January 31, 2015
Hizi ndivyo lori hilo lilivyoharibika
WATU watatu waliokuwa wamepakizana mishikaki wamekufa kwa kuteketea kwa moto mjini Iringa usiku huu baada ya usafiri aina ya pikipiki (Boda boda)waliyokuwa wakisafiri kutoka mjini Iringa kuelekea Nduli nje kidogo na mji wa Iringa kugongana na lori aina ya fusu na kupelekea pikipiki hiyo kuwaka moto.
| Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya Lori na boda boda leo usiku |
| Hii ndio pikipiki iliyoteketea kwa moto baada ya ajali |
Ajali hiyo
imetokea majira ya saa 2 usiku
huu wakati boda boda hiyo
ikiwa katika mwendo mkali
kugongana na lori hilo
ambalo pia lilikuwa katika mwendo na kusababisha
vifo hivyo .
Mashuhuda
wa
tukio hilo waliozungumza na mtandao
huu wa www.paparazihuru.com wamesema
kuwa kijana mmoja
ambae inasadikika ndie
dereva wa boda boda
hiyo ametambuliwa kwa jina moja la
Julius huku wengine wawili
bado kutambuliwa .
Kutokana
na ajali
hiyo mbali lori hilo upande wa mbele ngao yake
ilipinda huku eneo
hilo la mbele likiharibika vibaya
mfano wa kugongana gari kwa gari na baada ya
hapo pikipiki hiyo
ilishika moto na kuteketea
yote pamoja na watu hao ambao
miili yao ilizimwa kwa mchanga
na wasamaria wema.
Miili ya
marehemu hayo imehifadhiwa
katika chumba cha maiti
cha Hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Iringa
kwa utambuzi zaidi