WAZIRI LAZARO NYALANDU AZUNGUMZIA TETESI ZA KUTANUA NA AUNT EZEKIEL NCHINI MAREKANI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/waziri-lazaro-nyalandu-azungumzia.html?m=0
Baada
ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu Waziri wa Maliasili na Utalii
Lazaro Nyalandu(Pichani juu) na msanii wa filamu Aunty Ezekiel kuvinjari
nchini Marekani hatimaye waziri huyo amefunguka.
Nyalandu
alisema tuhuma hizo zimetengenezwa na kundi la watu ambalo miongoni
mwao ni baadhi ya viongozi wa Serikali ambao humchafua kutokana na
utendaji kazi wake.

Aunt Ezekiel
Nyalandu
alisema alikwenda Marekani septemba12 kwa ajili ya kufungua tamasha la
utamaduni na utalii kupitia soko la wasanii wa Tanzania ambako alikutana
na msanii huyo mara moja pamoja na mwingine wa Bongo Fleva Kassim
Mganga usiku katika moja ya maeneo nchini humo.
Alikana
kutanua na msanii huyo kama baadhi ya nyombo vya habari vilivyoripoti
na kusema maneno hayo ni kwa lengo la kumwaribia heshima yake mbele ya
jamii.