UHOLANZI YAUA 3-1 KUFUZU EURO
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/uholanzi-yaua-3-1-kufuzu-euro.html
NAHODHA Robin van Persie ameifungia
Uholanzi
ikipata ushindi wa kwanza katika mechi tatu chini ya kocha Guus
Hiddink tangu arithi mikoba baada Louis Van Gaal, baada ya kuifunga
Kazakhstan mabao 3-1 katika mechi ya Kundi A kufuzu Euro 2016.
Kazakhstan
walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Rinat Abdulin dakika ya 18
kabla ya Klaas-Jan Huntelaar kusawazisha dakika ya 62.
Wageni
walipata pigo baada ya mchezaji wao, Bauyrzhan Dzholchiev kutolewa kwa
kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumchezea rafu Ibrahim Afellay
dakika ya 64.
Afellay akaifungia Uholanzi bao la pili dakika ya 82 kabla ya Robin van Persie
‘kuunenepesha’
ushindi kwa bao la dakika ya 89 kwa penalti. Katika mechi nyingine
za Kundi A, Iceland imepata ushindi wa ugenini wa 3-0 dhidi ya Latvia na
Jamhuri ya Czech
imeshinda ugenini pia 2-1 dhidi ya Uturuki.
