REAL MADRID YAJIPANGA KUMNG’OA DE GEA MANCHESTER UNITED
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/real-madrid-yajipanga-kumngoa-de-gea.html
REAL Madrid
inajiandaa kuifanyia ‘fujo’ Manchester United kwa kuandaa mipango ya
kumnasa kipa David de Gea.Kumekuwa na msukumo mkubwa wa De Gea mwenye
umri wa miaka 23 kumrithi kipa Iker Casillas kwenye timu ya taifa ya
Hispania.Real Madrid nao pia wanadaiwa kuwa na mipango ya kufuata nyayo
za mageuzi yanayofanyika kwenye lango la timu ya taifa kwa kuangalia
uwezekano wa kumyakua De Gea.
Hata
hivyo United nayo iko mbioni kuendelea na maongezi ya mkataba mpya na
kipa huyo aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka Old Trafford msimu
uliopita.
De Gea aliyesajiliwa kwa pauni milioni 17.8 juni 2011 ana mkataba utakaomalizika mwaka 2016.
United
tayari ilishaanza gumzo la mkataba mpya na De Gea, lakini ikasitisha
kwa muda ili kupata wasaa wa kufanya kwa makini usajili wa dirisha la
kiangazi.
Real
Madrid inamuona kipa huyo wa zamani wa Atletico kama suluhisho pekee la
kuziba nafasi ya Casillas kama alivyofanya kwenye mechi ya Hispania ya
ushindi wa 4-0 dhidi ya Luxembourg.