Siku hizi ni tofauti kabisa na zamani ambapo tumezoea kuona watu wazima/wazee peke yao ndio watu wenye uwezo mkubwa na nguvu sana kwa hap...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/09/wajue-celebrity-vijana-wenye-nguvu.html
Siku hizi ni tofauti kabisa na zamani ambapo tumezoea kuona watu
wazima/wazee peke yao ndio watu wenye uwezo mkubwa na nguvu sana kwa
hapa Tzee,siku zinavyozidi kuendelea mambo yanazidi kubadilika na siku
hizi vijana ndio watu wanao-hustle juu chini kuweza kupata success hata
zaidi ya wazee wao waliotangulia,kwa hapa Tzee tumeweza kupata baadhi ya
vijana maarufu ambao ni most powerful na wenye influence kubwa kwa
vijana wenzao.
DIAMOND PLATNUMZ
Jina lake halisi ni Naseeb Abdul,so far ni msanii anayelipwa zaidi
kuliko msanii yeyote wa bongo fleva hapa Tzee,na kuongoza kulipwa zaidi
katika show zake za nje na ndani ya nchi.ukimuongelea Diamond platnumz
hivi sasa Africa lazima utakuta idadi flani hivi ya watu wanamfahamu
msanii huyu na hiyo ni mbali na huko ulaya na kwingineko duniani,ameweza
kufanya kazi zake za muziki na wasanii wakubwa duniani na kuweza
ku-share stage moja na wasanii akiwemo rick ross,Ludacriss ,Psquare na
wengine wengi,mbali na muziki pia ni ambassador wa cocacola
zero,goodwill ambasador wa malaria na ni moja ya wasanii wanaosaidia na
kujitolea katika shughuli mbalimbali za kusaidia jamii.
FLAVIAN MATATA
Kutoka mshindi wa kwanza wa miss universe Tanzania mwaka 2007 na kwenda
kuiwakilisha tanzania mwaka huo huo,Flaviana aliweza kuingia kwenye top
15 , kuingia nusu fainali na baadae kushika nafasi ya Sita na ndiye
aliyekuwa mtanzania wa kwanza kushiriki mashindano hayo ya miss universe
huku akiwa amenyoa nywele zake tofauti na washiriki wenzake,it was a
game changer kwa jina la Tanzania kujulikana kuwa kuna vipaji vingi
vilivyofichika.
Matata ameshiriki katika matangazo mengi sana akiwa kama model,mwaka
2011 aliweza kushinda tuzo ya model of the year award ya Arise magazine
ya huko nchini Lagos Nigeria,ametokea katika magazine mbalimbali duniani
yakiwemo Dazed & Confused, Glass Magazine, L’Officiel and i-D
Magazine. mbali na advertisement amefanya modeling ya mavazi ya brand za
wanamitindo maarufu duniani kama Mustafa Hassanali, Vivienne Westwood,
Tory Burch, Suno, na Louise Gray,pia kushirikishwa katika picha za
kutangaza collection ya mwanamitindo maarufu duniani , Alexander McQueen
katika Topshop Spring 2011 ad campaign.Flaviana matata baada ya
kuchukua tuzo ya “Face of Africa” aliweza kuwasaidia wanawake wenzake na
anaendelea na kampeni yake katika kusaidia wasichana waweze kwenda
shule kupitia foundation yake, Flaviana foundation.amekuwa ni kioo cha
wanawake na vijana wengi sana hapa Tzee.
JANUARY MAKAMBA
Huwezi kutaja list hii na kumuacha mtu huyu maarufu sana na ni role
model wa vijana wengi sana hapa nchini kwa yale aliyoweza ku-achieve
katika umri wake huo mdogo,unaambiwa alikuwa msaada mkubwa sana katika
serilkali ya Raisi.Kikwete toka mwaka 2005,mbali na hayo aliweza kupata
kiti cha ubunge kupitia jimbo lake la Bumbuli kupitia chama chake cha
CCM,nafasi aliyoweza kuipata kwa asilimia 80% kati ya wapinzani wake
nane,hii inaonyesha kuwa ni moja ya kijana anayeaminika sana na kupendwa
sana na wananchi,huyu ni moja kati ya waheshimiwa wanaopenda
ku-socialize sana na watu wa hadhi mbali mbali,na wa aina tofauti kitu
kinachozidi kumfanya kukubalika sana na vijana wenzake pia kumsaidia
kujua matatizo yao na jinsi yakuwapatia suluhu.
HASHEEM THABEET
Jina lake halisi ni Hashim Thabeet Manka ila maarufu kama Hashim Thabeet
tu,ni moja kati ya basketballer professional duniani anayeichezea timu
ya Oklahoma City Thunder.ni vigumu sana kuamini kwa mchezaji maarufu wa
huko NBA kutoka hapa hapa kwetu Tanzania,huyu ni moja kati ya wachezaji
warefu sana maarufu katika ligi ya mpira huu wa kikapu wa huko
marekani,ni moja kati ya wanamichezo wanaolipwa kuliko yeyote kutoka
hapa Tanzania na hata baadhi ya nchi,za hapa east Africa,na ni moja kati
ya celeb wakubwa sana hapa Tzee wanaojishughulisha sana na kazi
zakujitolea kwa jamii.
LADY JAY DEE
Ni moja kati ya wanawake wenye majina makubwa sana hapa mjini,ikiwa ni
msanii mkubwa sana wa kike anayeheshimika kutokana na kazi zake nzuri za
kimuziki, anamiliki biashara mbalimbali hiyo ni mbali kabisa na muziki
unaosemekana unamuingizia hela nyingi sana,mbali na muziki pia ni
mjasiliamari mkubwa sana,akiwa ni CEO wa Nyumbani Lounge ,Studios na
biashara nyingine nyingi,she is a hustler.ukimuongelea lady jay dee ni
msanii wa kike mwenye umaarufu na utajiri mkubwa, anapendwa na kila mtu
na kukubalika sana kimuziki na nje ya mziki huu wa Bongo fleva.
ZITTO KABWE
Jina lake halisi anaitwa Kabwe Zuberi Zitto ila maarufu anajulikana tu
kama Zitto Kabwe,huyu ni mmoja wa wanaharakati wanaojitahidi kutetea
haki za wananchi bila kuficha lolote lile kwa hadhira,ni moja ya tunda
litokalo kwenye chama cha demokrasia,pia ni mheshimiwa mbunge wa jimbo
la huko kigoma,ni moja kati ya vijana wenye umri mdogo na kuweza
kutikisa sana nchi haswa kwa hoja zake,umahiri wake kisiasa ndio moja ya
vitu vinavyopelekea kuzidi kupendwa sana na wananchi na hasa katika
swala zima la kutetea haki za wananchi,ni kijana hodari sana inapokuja
kwenye swala zima la siasa.
PATRICK NGOWI
Ni baada tu ya kuona kuwa kulikuwa na umuhimu wa kupata plan B ya umeme
hapa Tzee,Patrick aliamua kuachana na biashara ya kuuza simu na kuanza
kuingiza umeme wa solar hapa Tzee kwa mtaji mdogo tu na baadae kuzidi
kukua huku wananchi kuweza kupata suluhisho la tatizo lao la umeme hasa
kule kulipokosekana tumaini la kuwa na umeme,hivi ndivyo alivyoanza
kujipatia umaarufu mkubwa na biashara kukua sana kupitia kampuni yake
inayoitwa Helvetic Solar Contractors,kampuni iliyongezeka thamani na
kufikia zaidi ya dola milioni tatu kwa mwaka,hawa ni moja kati ya vijana
walioweza kutumia fursa.
OSSE GRECA SINARE
Talking about photographers maarufu sana hapa Tanzania na nje ya
Tanzania,Osse is the name to be mentioned, Jina lake na kazi yake
imeweza kutambulika na mataifa mbali mbali hata nje ya Tanzania,na
kuweza kuongelewa na baadhi ya majarida na mitandao mikubwa sana ikiwemo
Africa-vogue,fashion Ghana.com ,FAS mgazine na Msongo,si tu hapo pia
ameweza kufanya interview nyingi sana na media kubwa africca ikiwa
inaongelea kazi zake kwa kutambua uwezo wa kazi zake,mwaka 2012 aliweza
kupikea tuzo kutoka Swahili Fashion Week tuzo ya Best Fashion
Photographer,pia hujishughulisha na kazi za kusaidia jamii katika kuleta
mabadiliko katika maisha ya jamii zetu za hapa Tanzania