PICHA; ZA CHEMBE! AUNT EZEKIEL, HIVI KWELI WEWE NI MKE WA MTU?
https://samchardtz.blogspot.com/2014/09/picha-za-chembe-aunt-ezekiel-hivi-kweli.html
NIMEWAHI kuzungumza
mara kadhaa katika safu hii kuhusu huyu binti, mtoto wa nguli wa zamani
wa soka Tanzania, Ezekiel Greyson ‘Jujuman’, aliyevuma sana akiwa na
Simba. Anaitwa Aunt Ezekiel, staa wa filamu za Kibongo!
Nilisema
kuwa katika tasnia ya filamu, ni muigizaji mzuri kwa kupamba sinema
kutokana na uzuri wa sura na umbo lake, lakini katika wasanii
wanaotakiwa kwa weledi na viwango, bado ni mtu wa kati, ingawa akiwa
makini zaidi katika kazi yake, anaweza kuja juu!
Aunt,
kama walivyo wasanii wenzake wenye majina, anavuma zaidi nje ya fani
kuliko ndani. Wakati waigizaji kama Natasha, Aisha, Monalisa na Nora
enzi zao walivuma kutokana na uwezo wao katika kazi wakiwa na makundi
yao runingani, kizazi cha kina Aunt Ezekiel kinatikisa anga kikiwa
katika kumbi za starehe na kwenye mikusanyiko ya watu!
Leo
nazungumza tena na Aunt, hasa baada ya kujiuliza kwa muda mrefu na
kushindwa kupata jibu, la kama muigizaji huyu yupo katika ndoa au
alishaachika tena. Kumbukumbu zinaniambia aliwahi kuishi kwa kupika na
kupakua na mtoto mmoja wa mjini, Jack Pemba na baadaye Hartman Mbilinyi
kabla ya ndoa yake ya mwisho akiwa na Sunday Demonte.
Ingawa
ni vigumu kuthibitisha, lakini ushahidi wa mazingira unaonyesha Aunt
Ezekiel ni mmoja wa waigizaji wa kike ambao hawajatulia. Msanii huyu
anadai yupo katika ndoa na mumewe Demonte, ambaye anaelea katika uvumi
kwamba huko aliko, yupo matatizoni.
Ni
kipindi kirefu tokea mumewe alipoondoka nchini kuelekea Ughaibuni.
Sipendi sana kumuongelea yeye kwa sababu hayo ni masuala ya kibinafsi,
lakini hili la Aunt linanipa ugumu kidogo kulikalia kimya.
Aunt
anadaiwa kutoka kimapenzi na bwana mdogo mmoja mcheza shoo wa Diamond,
anayeitwa Moses Iyobo. Mapenzi yao yalianza kwa siri, lakini wenyewe
mara kadhaa kwa nyakati flani wamewahi kunukuliwa wakisema kuwa
hawaachani ng’o!Iyobo anadaiwa pia kuwa na mke, ambaye aliwahi hata
kuleta kasheshe kubwa baada ya kubaini uhusiano huo.
Ninajiuliza,
Aunt ameolewa, shemeji na wifi zake wapo hapahapa mjini, inakuwaje
anafanya mambo hadharani namna hii?Anyway, huenda basi hayo ni mambo ya
familia, wanajuana wenyewe, lakini kwa jamii inayomtazama huyu binti,
hasa watoto, anaifundisha nini kuhusu maisha ya ndoa?
Kwamba
unaweza kumuacha mumeo Mwanza, ukaja Dar es Salaam na kutanua tu ovyo
na waume wa wenzio? Huenda, kama ni kweli kwamba mumewe yupo matatizoni,
kama binadamu anaweza kujikuta akiwa na mahitaji ya kimaumbile.
Kama
ni hivyo, sasa kuna tatizo gani kufanya kwa siri? Watu kibao tu
wanafanya michepuko nje ya ndoa, lakini si wanafanya kwa kujificha ili
kulinda heshima ya familia zao?
Lipo
tatizo la msingi ambalo linapaswa kurekebishwa na huyu dada haraka.
Kama ametengana na mumewe, aweke hadharani ili kupunguza maswali haya,
kwa vile mashabiki wake na wale wa fani yake kwa jumla, wajifunze nini
kwake, kwamba unaweza kuolewa au kuoa na wakati huo huo ukawa huna hofu
na penzi lingine?
Hapana,
huu ni uhuni usiokubalika. Kuoa au kuolewa kunamaanisha ni mwisho wa
maisha yako ya kutangatanga kingono, umeamua kutulia kwa mmoja
umpendaye. Kama alikuwa bado hajatosheka kwa nini alijiongopea?
Jambo
lingine la kumshauri ni kuwa umri unasogea, asije kujikuta anazeeka na
ujana bado haujamwisha, kwa sababu kwa jinsi anavyoyaendesha maisha
yake, ni kama vile nayo anaigiza kama anavyofanya kwenye filamu!
Bonyeza HAPA like page yetu