Pellegrini:ManCity itatetea taji lake
https://samchardtz.blogspot.com/2014/08/pellegrinimancity-itatetea-taji-lake.html
Kocha wa Manchester City
Manuel Pellegrini amesema anamatumaini makubwa timu hiyo italitetea taji
lake licha ya kuambulia kichapo cha mabao matatu kwa nunge dhidi ya
vibonde wao Arsenal katika mechi ya kuwania ngao ya Community hapo jana.
Man City, wameratibiwa kufungua kampeini ya kutetea taji lao dhidi ya Newcastle jumapili ijayo.'' Nafahamu kuwa msimu huu timu 5 au hata 6 zinauwezo wa kutwaa taji la ligi msimu huu lakini nakuhakikishia kuwa kati ya timu hizo zote Man city ndiyo inatimu yenye uwezo wa kushinda.'' alisema Pellegrini.
''Wajua ni vigumu kuamini lakini mkitupa muda tutawathibitishia hilo uwanjani''.
Man City iliambulia kichapo cha 3-0 dhidi ya Arsenal.
''Unafahamu kuwa kikosi kilichocheza hivi leo sio kikosi chetu cha kwanza ''.
Pellegrini alimpa nafasi ya kuanza mchezaji mpya Willy Caballeroin na akamwelezea kipa nambari moja msimu uliopita Joe Hart, kuwa lazima adhihirishe uwezo wake msimu huu kwani anaupinzani si haba.