WADADA KADHAA WACHEZEA KICHAPO KIKALI TOKA KWA MAUSTAADHI...WALIKUA WANAJIUZA
Maustadh wakimuadhibu mmoja wa machangudoa hao.
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/wadada-kadhaa-wachezea-kichapo-kikali.html
MAUSTADH jijini
Dar es Salaam wamefikia uamuzi mzito wa kutembeza bakora kwenye vijiwe
korofi vya warembo wanaojishughulisha na biashara haramu ya kuuza miili
almaarufu kama machangudoa au machangu kwa kile kilichodaiwa kuwa
wanasafisha jiji kutokana na kero za vishawishi vya kuharibiwa Mfungo wa
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kwa
mujibu wa sosi aliyewasiliana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya
Global Publishers, maustadh hao walianza oparesheni yao waliyoibatiza
jina la ‘Safisha Jiji’ maeneo ya Sinza kwenye mitaa ya Shule ya Msingi
ya Mapambano na jirani na msikiti uliopo maeneo ya Afrika Sana.
Wakati
maustadh hao wakiwafungia kazi na kutembeza bakora, OFM ilifika maeneo
hayo na kufanikiwa kunasa tukio zima ambapo iliwashuhudia warembo hao
waliokuwa wakijiuza kwa madai ya kusaka fedha za sikukuu, wakipewa
kibano cha kutosha.
Wakizungumza
na OFM baada ya sakata hilo, maustadh hao walisema wamechoshwa na
uchafu unaofanyika kwenye makazi yao huku wakifunguka kuwa mara kadhaa
wanaporudi nyumbani wakitokea msikitini, machangu hao huwang’ang’ania
wakiwashawishi kufanya nao ngono bila kujua wapo katika mfungo.“Tumechoshwa
na ufuska, mbaya zaidi hawa machangu wanafikia hatua ya kutung’ang’ania
wakitulazimisha tuwanunue bila kujali kama tunatoka msikitini kuswali,”
alisema mmoja wa maustadh hao na kuongeza kuwa wanauheshimu mwezi huu
mtukufu ndiyo maana wameamua kutembeza bakora kwa machangu hao.
Hahahaha Safi sana nidhamu ikae Pahala pake
ReplyDelete