UKRAIN KUJIBU MAPIGO
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/ukrain-kujibu-mapigo.html
Jeshi la Ukrain limeanza
kujihami mashariki mwa nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya waasi wa Urusi
kufuatia kutunguliwa kwa ndege ya Malaysia katika eneo hilo.
Msemaji wa serikali ya Ukrain Andriy Lysenko
amesema jeshi la nchi hiyo lilidhamiria kulifunga eneo hilo ili kupisha
uchunguzi wa watalaamu kuhusiana na chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo.Ndege ya Malaysia iliyokuwa imebeba watu 300 iliangushwa katika eneo hilo lililo chini ya udhibiti wa waasi.
Waangalizi wa kimataifa wanasema mapigano hayo yataadhiri uchunguzi wa ajali hiyo ya ndege, mapigano makali yameripotiwa katika amaeneo yanayozunguka mji wa Horlivka na Shakhtarsk.