TAASISI YA KUFUNDISHA HISABATI YAJA, MKATABA KUSAINIWA AGOSTI 4
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/taasisi-ya-kufundisha-hisabati-yaja.html
Serikali
inatarajia kusaini makubaliano ya awali (MOU) na Taasisi ya Masuala ya
Sayansi ya Hesabu Afrika (AIMS), yatakayoiwezesha taasisi hiyo
kuanzisha kampasi yake hapa nchini itakayofundisha na kuendeleza masomo
ya Hisabati na Sayansi.
Katika taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylivia Temu, mkataba huo utasainiwa rasmi Agosti 4, mwaka huu.
Alisema kampasi hiyo itakuwa ya tano kuanzishwa na taasisi hiyo katika mataifa mbalimbali na itasaidia kuandaa wataalamu wa kuendeleza masomo ya Hisabati na Sayansi nchini kwa njia tofauti, ikiwa ni pamoja na ufundishaji wa masomo hayo kwenye ngazi mbalimbali za elimu.
“Kuanzishwa kwa kampasi hiyo ni jitihada za Rais Jakaya Kikwete, aliyekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa AIMS, Profesa Nell Turok, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Perimetr Institute for Theoretical Physics, ambayo ina uhusiano na AIMS,” alisema Profesa Temu.
Alisema Profesa Turok ni mzaliwa wa Afrika Kusini na ni mtoto wa Ben Turok, mpigania uhuru wa nchi hiyo ambaye ni mbunge na aliwahi kuishi Tanzania wakati wa utoto wake.
Kwa mujibu wa Profesa Temu, taasisi hiyo inayotoa shahada za utafiti kwa ngazi mbalimbali, inalenga kutoa wanafunzi wenye uwezo wa kufanya utafiti wenye ubora wa kiwango cha juu katika masuala ya sayansi.
Alibainisha kuwa AIMS imejikita kutoa mafunzo katika ngazi ya Uzamili kwenye sayansi za Hisabati na hadi mwaka 2013, taasisi hiyo ilishaanzisha vituo vinne Afrika katika nchi za Afrika Kusini, Ghana, Cameroon na Senegal.
“Serikali kwa kutambua umuhimu wa masomo ya Sayansi na mwitikio chanya uliopo sasa kwa wanafunzi kusoma masomo hayo, imeendelea kuimarisha miundombinu ya shule kwa kutoa fedha za ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa majengo ili wanafunzi wengi zaidi wasome masomo hayo,” alisema.
Serikali inafanya juhudi mbalimbali za kukabiliana na changamoto ya uhaba wa wataalamu katika fani za sayansi, kwa kujiwekea mkakati wa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi aliyefaulu masomo ya Sayansi, anapangiwa taasisi ya masomo ya Sayansi.