Rudisha ashindwa kuwika Monaco
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/rudisha-ashindwa-kuwika-monaco.html
Bingwa wa Olimpiki na
anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 David Rudisha
hakuweza kurudia alichofanya Glasgow wiki iliyopita katika mbio za mita
800, baada ya kushindwa na Nigel Amos wa Botswana aliyemaliza wa kwanza
kwa dakika moja sekunde 42.45.
Rudisha alimaliza katika nafasi ya tano, licha ya kuongoza mbio hizo kwa muda.Pierre-Ambroise Bosse wa Ufaransa alimaliza wa pili na Ferguson Rotich Cheruiyot akimaliza wa tatu.
Asbel Kiprop aliyesema atajaribu kuvunja rekodi ya Hicham El Gerrouj katika mbio za mita 1500, alishindwa kufanya hivyo na kumaliza nafasi ya pili, baada ya kupitwa na Silas Kiplagat katika mzunguko wa mwisho.