Marufuku ya Utumizi wa magari Nigeria
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/marufuku-ya-utumizi-wa-magari-nigeria.html
Jeshi la Nigeria limepiga
marufuku utumizi wa magari kwa siku tatu katika jimbo la Borno kaskazini
mashariki mwa taifa hilo ili kuzuia tishio la wanamgambo wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa hatua hiyo itazuia
utumiaji wa magari kutekeleza mashambulizi ya kujitolea mhanga wakati
wa siku kuu ya Eid ul Fitr.Wakati huohuo kumekuwa na ripoti ambapo mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua watu kadhaa katika mji wa kazkazini wa KANO.
Gavana wa Borno Kassim Shetima amesema kuwa anawaonea huruma maelfu ya watu waliolazimika kutumia mda wao mwingi kutembea hadi katika viwanja vya kufanyia salah,lakini akaongezea kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda .
Jeshi la Nigeria hivi majuzi lilikiri kwamba baadhi ya wanajeshi wake walikuwa wanatoroka kutokana na uvamizi wa wanamgambo hao.