Flatnews

KIZAAZAA: MAJAMBAZI YA KIKE YANASWA NA SILAHA NANE ZA KIVITA, FUKWE ZA BAHARI ZAWEKWA VITUO VYA POLISI VYA MUDA JIJINI DAR ES SALAAM.



 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata watuhumiwa 10 wa ujambazi, wakiwamo wanawake wawili waliokutwa na silaha nane za kivita kufuatia msako uliofanywa na jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema majambazi hao walikuwa katika mtandao wa ujambazi wa
kufanya uhalifu katika maeneo tofauti.

Alisema polisi wameimarisha ulinzi katika maeneo yote, ikiwamo katika nyumba za ibada kwa ajili ya Sikukuu ya Iddi El-Fitri kwa kushirikiana na vyombo vingine, vikiwamo Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji pamoja na kampuni binafsi za ulinzi.

“Tumejipanga kuimarisha ulinzi kutumia kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kwa kutumia magari maalumu, mbwa, farasi waliofundishwa ulinzi na usalama, kikosi cha wanamaji na wale wa usalama barabarani,” alisema Kamanda Kova.

Alisema polisi watatoa ulinzi katika fukwe za bahari kwa kuweka vituo vya polisi vya muda katika maeneo hayo ili kuhamasisha ulinzi ili kutoa msaada wa haraka utakapohitajika.

“Tunawaomba wazazi walezi kuwa makini na watoto, ambao wanahitaji kuangaliwa usalama wao katika fukwe za bahari na maeneo ya kuogelea, licha ya Jeshi la Polisi kuwapo katika baaadhi ya fukwe za bahari kuangalia ulinzi na usalama,” alisema Kamanda Kova. CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

emo-but-icon

item