WILAYA YA KALAMBO-RUKWA YAIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/wilaya-ya-kalambo-rukwa-yaimarisha.html
PICHA KWA HISANI YA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO
NA RAMADHANI JUMA
OFISI YA MKURUGENZI-KALAMBO
OFISI
ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa kupitia
kitengo cha UKIMWI kimetumia zaidi ya shilingi milioni 8.5 kwa ajili ya
kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo katika wilaya hiyo.
Fedha
hizo zimetumika kuwanunulia wanafunzi yatima wanaoishi katika mazingira
magumu sare za shule, viatu pamoja vifaa vya kujifunzia ikiwemo
madaftari na kalamu, ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Godfrey
Sichona alikabidhi kwa walengwa kwa niaba ya Halmashauri.
Pia
Halmashauri hiyo imenunua vifaa vya muziki kwa ajili ya vikundi viwili
vya Sayuni kilichopo kata ya Legezamwendo na Sayuni cha Kata ya
Mambwenkoswe ili vihamasishe wananchi kujikinga na ugonjwa huo.
Baadhi
ya vifaa vya muziki vilivyotolewa na Halmashauri hiyo ya Kalambo ni
gitaa tatu kila kikundi, spika, maikrofoni, genereta pamoja na vifaa
vingine vya umeme.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi misaada hiyo, mwenyekiti huyo aliwakumbusha wakazi
wa wilaya ya Kalambo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla kuwa, mapambano dhidi
ya UKIMWI sio ya serikali pekee bali ni jukumu la kila mwanajamii
zikiwezo taasisi za dini.
Naye
mwenyekiti wa kamati ya Kudhibiti UKIMWI wilaya ya Kalambo Faustine
Mwanisenga aliwataka wanavikundi waliopatiwa msaada wa vifaa vya muziki
na Halmashauri hiyi kuvitunza na kuvitumia vizuri ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.