TUZO ZA MTV SAUZI, DIAMOND MUMUACHE
WAMUACHE! Hii ndiyo kauli pekee ambayo unaweza kuisema kwa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwani Jumamosi iliyopita alifanya maajab...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/tuzo-za-mtv-sauzi-diamond-mumuache.html
WAMUACHE! Hii ndiyo kauli pekee ambayo unaweza kuisema kwa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwani Jumamosi iliyopita alifanya maajabu na kuishangaza dunia kufuatia shoo kali aliyoangusha katika Tuzo za MTV Africa (Mama) 2014 katika Ukumbi wa ICC, Durban nchini Afrika Kusini.
Diamond
aliyeambata na timu ya wasanii tofauti kutoka Bongo wakiwemo waigizaji
na mameneja wake, licha ya kukosa tuzo alizokuwa akiwania yaani
kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kiume na Wimbo Bora wa Kushirikiana,
alikuwa gumzo kwa kupiga shoo kali akishirikiana na David Adeleke
‘Davido’ wa Nigeria.
Awali, shoo
hiyo ilianza saa nne usiku ambapo Diamond aliyeambatana na ubavu wake,
Beautiful Onyinye, Wema Sepetu walikuwa kivutio katika ‘red carpet’
ambapo walipoingia wakiwa wamekumbatiana, watu walipiga kelele kuashiria
kuwa wanaikubali kapo hiyo.
Miongoni mwa shoo za awali ambazo ziliamsha hisia za mashabiki waliofurika ukumbini humo ni ya Kundi la Mafikizolo ambayo lilishangiliwa sana.
Miongoni mwa shoo za awali ambazo ziliamsha hisia za mashabiki waliofurika ukumbini humo ni ya Kundi la Mafikizolo ambayo lilishangiliwa sana.
Wa kwanza
kunyakua tuzo ya Mwanamuziki Bora Chipukizi ni Stanley Enow wa Nigeria.
Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike ilienda kwa Tiwa-Savage wa Nigeria na
Mwanamuziki Bora wa Hip Hop ilienda kwa Sarkodie wa Ghana. Muonekano wa
Jumla, tuzo ilitua kwa mwanadada Lupita Nyong’o wa Kenya.
Kwenye
kipengele cha Kundi Bora la Mwaka, tuzo ilikamatwa na Mafikizolo ambao
waliwatupa kapuni P- Square, Sauti Sol, Mi Casa na Big Nuz.
Davido
aliibuka Mwanamuziki Bora wa Kiume wa Mwaka na kuwagalagaza akina
Diamond, Wizkid, Anselmo Ralph na Donald. Kipengele cha Wimbo Bora wa
Kushirikiana, tuzo ilitua kwa Uhuru aliyeshirikiana na DJ Buckz, Oskido,
Professor na Yuri da Cunha.
Hapo ndipo
alipopanda mkali kutoka Marekani, Trey Songz ambaye alipewa shangwe za
kutosha hususan alipopiga wimbo wake wa Nana kisha jukwaa likakamatiwa
na Diamond na Davido ambao walipafomu wimbo wa Number One Remix ambapo
mtoto huyo wa Tandale alipagawisha mashabiki wote kwa kuonesha staili
tofauti za kucheza kabla ya kumuacha stejini Davido aendeleze makamuzi.
Diamond na
Davido waliingia kwa staili ya aina yake ya kuzuiwa na warembo mlangoni,
wakavamia jukwaa kwa spidi na kufanya umati uwe bize kwa dakika kadhaa
wakati shoo hiyo ya nguvu ikiendelea.