Sudan Kusini yailaumu Kenya kumpokea Machar
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/sudan-kusini-yailaumu-kenya-kumpokea_9.html
Kiongozi
wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar (R) na Rais wa Sudan Kusini Salva
Kiir wakibadilishana mkataba wa amani huko Addis Ababa, Ethiopia
Sudan
Kusini inadai kwamba Sudan inajaribu kuhujumu uhalali wa serikali ya
Rais Salva Kiir na uhusiano kati ya mataifa hayo mawili baada ya
wawakilishi wa waasi wanaomtii Makamu Rais wa zamani Riek Machar
waliporuhusiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari katika nchi hiyo
jirani mwishoni mwa wiki.(Martha Magessa)
Msemaji
wa rais wa Sudan kusini Ateny Wek Ateny pia alitoa lawama kama hizo kwa
Kenya kwa kumpa Machar mapokezi yenye hadhi ya kiongozi ya zulia jekundu
kufuatia mkutano wake wa hivi karibuni na Rais Uhuru Kenyatta kama
juhudi za Nairobi za kutatua mzozo wa Sudan Kusini.
Amesema
"Kwa serikali ya Kenya kumpokea kiongozi wa waasi kwa heshima za zulia
jekundu ni tusi kwa uhuru wa Sudan Kusini. Upinzani haupokelewi kwa
zulia jekundu wakati wanapotembelea nchi za nje, alisema Ateny".
Aliongeza
kusema "kama Raila Odinga, Makamu Rais wa zamani wa Kenya anakuja Sudan
Kusini hatuwezi kumwekea zulia jekundu, kwa nini Kenya wanafanya hivyo?
Kwa sisi ni kuitusi Jamhuri ya Sudan Kusini".
"Kama
Rais wa Kenya alikuwa mwenyeji wa kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini kwa
misingi kwamba alikuwa Makamu Rais wa zamani, basi ingefaa William
Rutto- Makam Rais wa Kenya angetakiwa kufanya hivyo, alisema Ateny.
"Hili ni
jaribio la kuhujumu uhalali wa serikali ya Juba," alisema Ateny.Matamshi
ya Ateny yalifuatia mkutano wa wajumbe wa waasi na waandishi wa habari
katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum. Ujumbe ulikuwepo Sudan kama sehemu
ya maandalizi ya ziara ijayo ya Riek Machar huko Sudan.
CHANZO:VOA