Sanusi achaguliwa Emir mkuu wa Kano
Sanusi sasa ndiye Kadhi mkuu wa Kano
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/sanusi-achaguliwa-emir-mkuu-wa-kano.html
Aliyekuwa Gavana mkuu wa benki kuu ya Nigeria , Lamido Sanusi, ametajwa kuwa kadhi mpya wa Kano nchini Nigeria.
Kadhi huyo mpya aliyejiwekea taji la kuwa
mhakiki mashuhuri wa serikali atakakuwa miongoni mwa viongozi wa dini
wenye ushawishi mkubwa kaskazini mwa taifa hilo .Aliyekuwa kadhi hapo awali, Al-Haji Ado Bayero, aliaga dunia akiwa na miaka 83 Ijumaa baada ya kuugua kwa muda mrefu
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC aliyeko Abuja Tomi Oladipo, Bwana Sanusi alifanya mageuzi alipokuwa gavana wa benki ya taifa , akikabiliana na ulaghai ulioenea katika sekta ya fedha.
Sanusi sasa ndiye Kadhi mkuu wa Kano
Rais Goodluck Jonathan hakufurahishwa na madai hayo na hivyo kibarua chake bwana Sanusi kikaota nyasi katika benki kuu.
Kama kadhi mpya wa Kano, uhusiano kati ya Lamido Sanusi na rais Jonathan utaangaliwa kwa makini kabla ya uchaguzi wa urais mwaka ujao.
Mojawapo ya kazi ya bwana Sanusi itakuwa kusaidia kukabiliana na uasi wa kundi la wanamgambo wa Boko Haram kasazini mwa nchi hiyo.
Kundi hilo limewashutumu viongozi wa dini ya Uislamu kwa kushindwa kutekeleza tafsiri kali ya Koran.