Flatnews

Rais Obama ashiriki sherehe za D-Day Ufaransa

Rais Barack Obama na Francois Hollande wa Ufaransa katika maadhimisho miaka 70 ya Vita vya Pili vya Dunia, Normandy, Ufa...



Rais Barack Obama na Francois Hollande wa Ufaransa katika maadhimisho  miaka 70 ya Vita vya Pili vya Dunia, Normandy, Ufaransa
Rais Barack Obama na Francois Hollande wa Ufaransa katika maadhimisho miaka 70 ya Vita vya Pili vya Dunia, Normandy, Ufaransa


ukubwa wa habari
White House inasema Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa Russia Vladmir Putin walizungumza kwa muda mfupi kwenye sherehe za maadhimisho ya D-Day nchini Ufaransa licha ya  tofauti zilizopo juu ya Russia kujiingiza katika  peninsula ya Crimea huko Ukraine.

White House ilisema viongozi hao wawili walikuwa na mazungumzo  yasiyo rasmi Ijumaa  ambayo yalidumu kwa dakika 10 hadi 15 wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa na mwenyeji wao Rais wa Ufaransa, Francois Hollande.

Awali, Rais Obama alitoa heshima kwa wanajeshi wakongwe wa Vita vya Pili vya Dunia kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 70 uvamizi ambao ulipelekea kuwashinda wajerumani wa Nazi.

Katika hotuba yake huko Omaha Beach kwenye mwambao wa Normandy, Ufaransa, bwana Obama aliwapongeza  wanajeshi ambao alisema walitoa maisha yao  kwa ajili ya ukombozi  wakati wa kipindi cha hatari sana.

Kiasi cha wanajeshi 160,000 wa ushirika walivuka kwenye maji ya Normandy hapo Juni 6 mwaka 1944 ambapo lilikuwa shambulizi kubwa kabisa la baharini katika historia ya jeshi. Japokuwa kiasi cha wanajeshi 4,500 walikufa wakati huo, operesheni hatimaye ilipelekea ushindi wa majeshi ya ushirika kote ulaya.

Katika hotuba yake Rais Obama aliwapongeza  wanajeshi wa zamani ambao walishiriki kwenye D-Day kwa kubadilisha mwelekeo wa historia ya binadamu.

Katika sherehe za ufunguzi Rais wa Ufaransa Francois Hollande pia alisema kujitoa kwa wanajeshi hao “kumeibadilisha Dunia”.

Post a Comment

emo-but-icon

item