PENY,JOKATE NA WOLPER WATOA SABABU ZILIZO WAFANYA KUACHWA NA DIAMOND,SOMA HAPA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/penyjokate-na-wolper-watoa-sababu.html
Hadi
hii leo Divas maarufu waliowahi kufunguka kiundani kuhusu kutoka na
mwanamuziki huyu, na kwa nyakati tofauti kila mmoja wao alijaribu
kufunguka kuhusu experience zao, pindi walipokuwa wanatoka na mkali wa
bongo fleva nchini hivi sasa Mr.Dangote aka Diamond Platnumz, ambaye
amerudiana na kuendelea kudumu katika penzi lake la zamani na la siku
zote kwa Diva Wema Sepetu..basi haya ndo machache waliowahi kutoa ya
moyoni.
DVJ Penny
“Kama
uhusiano wowote ulivyo, kuna mwanzo na mwisho na watu wanaachana kwa
sababu nyingi. Nilihisi kwamba nahitaji kumpa nafasi, wote ni vijana na
wakati mwingine tunahitaji nafasi kugundua vitu vipya, kuona kipi hasa
unachokihitaji kwenye maisha. Unajua ukimruhusu ndege afanye vitu
mbalimbali then atajua kama ‘mti huu ndio
unanifaa, mti huu haunifai. Hivyo
nilihisi kwamba wote tulihitaji hicho, tulihitaji ‘space’ hivyo nikampa
nafasi na mimi nakuchukua nafasi. Huwa nawaambia watu kuwa vyovyote
ilivyo, yeyote atakayekuwa naye, nipo pembeni yake nikimshangilia
kwasababu ni kweli (Diamond) ni mtu mzuri ndani. Achana na watu
wanavyomuona chizi chizi, sahau msanii unayemjua, ana roho nzuri na
anajua anachokitaka. Ni ngumu kuacha iende.. kama ni rahisi kuacha iende
basi hujampenda huyo mtu.”
Jokate Mwegelo
“Mahusiano
ya diamond yalikuwa very strange, I dont know yani..i think ilikuwa
kazi lakini I guess it was a time I guess I was frustrated,sielewi yani
ilitokea tokea tu”
Jackline Wolper
“Ni
kweli niliwahi kuwa na diamond,tulikuwa na mahusiano lakini pia alikuwa
ni mshirika wa biashara,yeye alikuwa hawezi kulala bila kuniona,lakini
tulidumu kama mwezi mmoja hivi, tukaishia kuwa marafiki tu.