Oxfam yaanzisha Kombe la dunia mbadala
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/oxfam-yaanzisha-kombe-la-dunia-mbadala.html
Shirika la kutoa huduma za
kibinadamu Oxfam limeendesha kile inachosema ni 'kombe la dunia mbadala'
kuangazia pengo linalozidi kuwa kubwa kati ya maskini na matajiri
katika mataifa yanayoshiriki kombe la dunia mwaka huu.
Ubelgiji imetangazwa mshindi kwa sababu si kuwa
ina utajiri si haba bali pia ina mwanya mdogo zaidi kati ya raia wake
matajiri na wenye kipato, ilhali wenyeji Brazil imefeli hata kufuzu
raundi ya pili kwa jinsi pengo la umaskini na matajiri lilivyokumbwa
miongoni mwa raia wake.Mataifa mengineyo ya America kusini pia hayajafanya vizuri lakini yanasemekana kujitahidi, cha ajabu mataifa ya kiafrika yanayoshirki kombe la dunia hayajatajwa.