MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI UTAKAVYOWAATHIRI NYOTA WAISLAMU KOMBE LA DUNIA, UTAANZA SAMBAMBA NA RAUNDI YA PILI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mwezi-mtukufu-wa-ramadhani.html
BAADHI ya
nyota wanaotarajiwa kuziongoza timu zao kwenye Kombe la Dunia
wanatarajiwa kuwa na wakati mgumu mara utakapoanza mfungo wa mwezi
mtukufu wa Ramadhani.
Hii itakuwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986 ibada hiyo ya waislamu inakuja wakati wa mashindano hayo ya Kombe la Dunia.
Waislamu
wanafunga kutwa nzima wakati wa Ramadhani na hawaruhusiwi kula wall
kunywa wakati huo, hali ambayo itawaathiri wachezaji waumini wa dini
hiyo katika Kombe la Dunia.
Ramadhani
itaanza Juni 28 – siku ya kwanza ya Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia na
itakwenda hadi Julia 27 na nchi kama Ufaransa na Ivory Coast
zitaathirika zaidi zikiingia Hatua ya 16 Bora, kwani wachezaji wake
wengi ni waislamu safi.
Mtu na kaka yake: Wachezaji wawili ndugu wa Ivory Coast, Yaya (kushoto) na Kolo Toure ni waislamu safi
Mshambuliaji wa Uswisi, Xherdan Shaqiri ni Muislamu pia
Nyota wa Ufaransa akiwemo mshambuliaji wa Real Madrid’s Karim Benzema, Mamadou Sakho wa Liverpool, beki wa Arsenal, Bacary Sagna na Moussa Sissoko wa Newcastle wote Waislamu.
Wakati
huo huo, Ndugu wawili wa Ivory Coast, Yaya na Kolo Toure – wa Manchester
City na Liverpool pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho
na kiungo wa Newcastle, Cheick Tiote nao pia ni Waislamu safi.
Sehemu kubwa ya wachezaji wa Bosnia– akiwemo mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko –
ni Waislamu pia, sawa na wachezaji wawili wa Ubelgiji wanaocheza Ligi
Kuu ya England, Marouane Fellaini na Moussa Dembele, tegemeo la Uswisi,
Xherdan Shaqiri na kiungo Mjerumani wa Arsenal, Mesut Ozil.
Kitu
kimoja kizuri kwa wachezaji hao ni kwamba kwa sasa kutwa moja ina saa 11
mjini Rio de Janeiro, ukilinganisha na saa 17 za Uingereza.
Baadhi ya
wachezaji wa kiislamu huachana na ibada hiyo wakati wa mashindano,
lakini winging kama Kolo Toure, wan a msimamo mkali na huendelea
kufunga.
Mtu mkubwa: Nyota wa Ujerumani, Mesut Ozil ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa nchi yake