Mwanamke
mmoja mwenye umri wa miaka 19 amekutwa amening’inizwa juu ya mti katika
kijiji kimoja Kaskazini mwa India, likiwa ni tukio la tatu kutokea
ndani ya wiki moja katika Jimbo la Uttar Pradesh.Mwili wa
mwanamke huyo umekutwa katika eneo la Moradabad ambapo familia yake
imewaambia polisi kuwa alibakwa huku uchunguzi wa madaktari ukiendelea
kufanyika.Mwanamke mwingine alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika
Jimbo la Uttar Pradesh siku ya Jumatano.Mwezi uliopita mabinti wawili
wadogo walibakwa na kundi la watu katika mazingira kama hayo na kuibua
maandamano ya hisia kali nchini India.
Siku ya Jumatano, mwanamke mwenye umri wa miaka 44 nae alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika eneo la Bahraich.
Polisi
wamesema kuwa alikuwa akipatiwa vitisho na wanakijiji kwa kuuza pombe
katika eneo hilo na familia yake ilifungulia kesi watu watano kuhusiana
na kifo hicho.