MSAADA WA MATIBABU KWA MTOTO MAIMUNA YAHAYA (11)
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/msaada-wa-matibabu-kwa-mtoto-maimuna_9.html

Mtoto Maimuna Yahaya akiwa na Mama yake Mzazi Tunu Juma
Msaada
wa Matibabu kwa mtoto Maimuna Yahaya Mtoto Maimuna Yahaya (11)
anayesoma shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalum (wenye
ulemavu) ya Irente Rainbow (Lushoto- Tanga) Darasa la pili, anasumbuliwa
na tatizo la mifupa na ukubwa wa kichwa tangu kuzaliwa kwake, tatizo
lililompelekea kuwa na ulemavu wa viungo na mtindio wa Ubongo.
Mama
wa mtoto huyo, Bi. Tunu Juma Maziku amesema amekuwa akimpeleka mwanae
huyo Maimuna katika hospitali ya KCMC kwa muda wa miaka 11. Hali ya
mtoto inaendelea kuimarika, anaweza kukaa na anawezakuongea.