Flatnews

MKUTANO WA 64 WA FIFA WAFUNGULIWA SAO PAULO, BLATTER NA WAZIRI WA MICHEZO BRAZIL WAUNGURUMA.

    Mwimbaji wa Brazil,  Maria Rita (kushoto, mbele), mwanamitindo Fernanda Lima (kulia, mbele ) wakitumbuiza katika mkutano huo.



 
 Mwimbaji wa Brazil,  Maria Rita (kushoto, mbele), mwanamitindo Fernanda Lima (kulia, mbele ) wakitumbuiza katika mkutano huo.
SAO PAULO, Brazil
Rais wa shirikisho la soka duniani, FIFA,  Sepp Blatter amefungua mkutano wa 64 wa shirikisho hilo, mjini Sao Paulo jana jioni.
Maofisa wa juu wa FIFA, mashirikisho sita wanachama wa FIFA na wanachama 206 vya vyama walihudhuria mkutano huo.
Blatter pamoja na Wazili wa michezo wa Brazil, Aldo Rebelo walitoa hotuba zao kwenye mkutano huo wakizungumzia fainali zinazoanza kesho nchini Brazil.
Mkutano huo uliambatana na zawadi mbalimbali, burudani kutoka kwa wasanii na mambo yaliiva zaidi pale mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa mwenye miaka 80 kwa sasa, Just Fontaine alipozawadiwa kiatu cha Adidas chenye madini ya almasi.
Nyota huyo alifunga mabao 13 katika mechi sita za kombe la dunia lililofanyika nchini Sweden mwaka 1958 na kuiongoiza Ufaransa kushika nafasi ya tatu, huku akiibuka mfungaji bora wa pekee katika historia ya fainali za kombe la dunia. Rekodi yake haijavunjwa mpaka leo.
 
 Picha hii ilipigwa jana juni 10, 2014 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 64 wa  FIFA.
Kwa kuwa fainali za 1958 hazikuwa na zawadi ya kiatu cha dhahabu, Fontaine alisema jana usiku kuwa kiatu hicho ni zawadi maalum kwa mke wake na timu yake ya Ufaransa.
Muda wa jioni, wawakilishi mbalimbali, Josephine King (OFC), Hassan Shehata (CAF), Mirabror Usmanov (AFC), Jozef Venglos (UEFA), Maria Coto (CONCACAF), Carlos Valderrama (CONMEBOL) na Antonio Mattarese (FIFA) walipata nafasi kuzungumza machache.
Kabla ya kufungua mkutano huo, kamati ya utendaji ya FIFA ilikaa kikao mjini Sao Paulo na kuwahakikishia Brazil kuwa watapa msaada kamili kutoka shirikisho hilo na wana imani nao kwa uwezo mkubwa walioonesha kuandaa kombe la dunia linaloanza kutimua vumbi kesho mjini Sao Paulo.
Pia Kamati ya utendaji katika mkutano huo iliwasilisha kanuni 10 za mpira wa miguu wa wanawake ikihitaji zipitishwe.
 
 Mshambuliaji wa zamani wa Brazil, Edson Arantes do Nacimento "Pele" akijibu maswali mjini Sao Paulo
Kuhusu kashfa za rushwa wakati wa upigaji  kura ya kumpata mwenyeji wa fainali za kombe la dunia kwa mwaka 2022, kamati ya utendaji ilisema suala hilo liachwe katika kamati ya maadili ili imalize kazi yake kabla ya kutoa msimamo wake.
Pia mkutano huo ulibariki maamuzi ya kuzisaidia Bosnia na Herzegovina, Croatia, Romania na Serbia msaada wa dola za kimarekani milioni mbili ili kuimarisha miundombinu ya soka ambayo iliharibiwa na mafuriko makubwa siku za karibuni.
Pia kamati ilithibitisha kuwa Mexico itaibadili Canada katika fainali za Olympik za soka la vijana la wanawake zinazotarajia kufanyika China mwaka huu.
Mkutano huo wa FIFA unamalizika leo jioni.

Post a Comment

emo-but-icon

item