MISS IRINGA KUFANYIKA JUNI 20
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/miss-iringa-kufanyika-juni-20.html
Baadhi
ya washiriki wa redds miss iringa wakiwa katika picha ya pamoja kabla
ya mazoezi katika ukumbi wanakofanyia mazoezi hotel ya Gentle Hill
iliyoko mkoani Iringa.
HATIMAYE
kinyang’anyiro cha kumsaka Redds Miss Iringa kinatarajia kufanyika Juni
20 mwaka huu baada ya aliyekuwa mratibu wa kwanza Mohamed Mcholeka
kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na kushindwa kufanyika Juni 6
kama lilivyopangwa mwanzoni na Tanzania Daima kuwa la kwanza kuripoti
kuhusiana kutoweka kwa shindano hilo.
Waandaji
wa Redds Miss Tanzania chini ya Lino Agency Hashim Lundenga baaada ya
kugundua hilo wamempatia kibali cha kuandaa shindano hilo ambalo
lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa tasnia ya urembo na
kwasasa Redds Miss Iringa imepata mratibu mwingine ambaye ni kutoka
kampuni ya Chakudika Intertainment chini uongozi wake Victor Chakudika
ambaye ni Meneja wa kituo cha radio ya Nuru Fm ya mjini Iringa.
Akizungumza
na Tanzania Daima ofisini kwake jana Mkurugenz wa kampuni hiyo, Victor
Chakudika alisema maamuzi ya kuandaa shindano la Redds Miss Iringa kwa
lengo a kutopoteza vipaji vya mabinti waliokuwa tayari kushiriki
shindano hilo na kuondoa aibu ya mkoa wa Iringa kutopelekwa mwakilishi
katika shindano la Redds Nyanda za Juu ambako wamekuwa wakishiriki kila
mwaka.
Alisema
kuwa shindano la Redds Miss Iringa limekuwa chachu ya ajira kwa mabinti
wengi mkoani hapa kwa kuweza kutangaza vipaji vya washiriki
wanaojitokeza kushiriki kila mwaka.
Chakudika
alisema shindano hilo linatarajia kuwa la kisasa kutokana na maandalizi
yake kuendelea vyema na kuwataka wadau wa tasnia ya urembo ujitokeza
kwa wingi katika ukumbi wa St. Dominic likalofanyika shindano hilo.
“Kwa
kweli baada ya mratibu wa kwanza kukimbia kutokana na gharama za
uandaaji niliamua kuchukua jukumu hilo kulikomboa shindano hilo
lifanyike na warembo wengi wamejitokeza kushiriki miss iringa” alisema
Chakudika.
Aliongeza
kuwa hadi sasa warembo 12 wamejitokeza kushiriki shindano hilo na
wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Hotel ya Gentle hill ya mjini
hapa. Aidha msanii Mo Music anayetamba na wimbo wake wa ‘Basi
Nenda’ anatarajia kutoa burudani kali katika shindano hilo ,wasanii
wengine chupukizi wa mjini Iringa, vikundi vya sanaa, Wakali wa Kudance
wa mjini Iringa.
Aliwataja
wadhamini wa shindano hilo licha ya TBL kupitia kinywaji chake cha
Redds, wengine ni Nuru Fm, kampuni mpya ya mabasi ya Sutco High Class,
Gentle Hills na kuwataka wadau zaidi kujitokeza kudhamini shindano hilo.