Makali ya magonjwa, kero duniani
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/makali-ya-magonjwa-kero-duniani.html
Kukosekana kwa fursa ya kupata
dawa za kupunguza uchungu au makali ya magonjwa yasiyo na tiba kwa
wagonjwa mahututi ni ''jambo ambalo linapuuzwa sana,” wasema wataalamu.
Takwimu zinaonyesha kuwa watu milioni 18- hasa
kwenye mataifa yanayokua- walikufa kutokana na uchungu ambao ungezuilika
mwaka wa 2012, huku kukiripotiwa kuwa wagonjwa wa Saratani nchini
Ethiopia walijirusha mbele ya malori ili kuepuka uchungu.Unaongeza kuwa vikwazo vimewekwa kwa hofu ya wagonjwa kutawaliwa na madawa hayo.
Mwezi uliopita, maafisa wa afya kutoka mataifa yapatayo 200 walikutana katika makao ya UN na kuahidi kuipa kipaumbele mpango wa kupunguza makali kwa wagonjwa wenye maradhi yasiyotibika.
Betty Naiga mwenye umri wa miaka 48, aliyepimwa na kupatikana na ugonjwa wa saratani na ambaye ni mkazi wa kijiji kidogo cha wilaya ya Wakiso nchini Uganda, analala kwenye godoro dogo sakafuni katika chumba chake kidogo cha manjano.
Betty aliishi kwa uchungu hadi alipokutana na Allen, mhudumu wa kujitolea katika huduma za kuwasaidia wagonjwa wenye magonjwa yasiyo na tiba kutoka hospitali ya Afrika Uganda.
'Mateso'
Baada ya hospitali hiyo kujihusisha na afya yake, Betty alipata fursa ya kupata matibabu ya Chemotherapy na kwa hivyo akahitaji dawa ya kupunguza makali ya Morphine.
''Maisha yangu yamebadilika pakubwa sana tangu nilipoanza kupata matibabu. Madawa yalisaidia kupunguza maumivu yangu,” alisema Betty.
Uganda inaongoza barani Afrika kwa huduma hizi za kuwasaidia wagonjwa mahututi.
Mataifa mengine kama vile Libya na Afganistan, hayapeani huduma hizo za kutuliza maumivu.
Huko Pakistani, zaidi ya watu 350000 walihitaji aina hii ya huduma katika mwaka wa 2012, lakini walioweza angalau kuipata ni takriban 300 tu, kulingana na takwimu zilizoonyeshwa BBC.
Kulingana na WPCA, kuna tu huduma mbili kama hizo zinazotolewa katika nchi hiyo nzima.
Huduma moja iliyoko Msumbiji iliwasaidia watu 153 pekee, kati ya 100,000 walihitaji huduma hiyo ya kupunguza makali katika mwaka wa 2012.