Maaskofu waikosoa serikali Eritrea
Kanisa katoliki nchini Eritrea
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/maaskofu-waikosoa-serikali-eritrea.html
Maaskofu wanne wa kanisa
katoliki nchini Eritrea,wamechapisha barua inayokosoa mfumo wa maisha
nchini humo, hatua ambayo inaonekana kama ya kishujaa ndani ya nchi
ambayo uhuru wa kujieleza umebanwa mno.
Ingawa maaskofu hao walijizuia na kulaani au
kukosoa serikali, hatua yao pekee ya kuandika barua hiyo inasemekana
kuwa hatua kubwa na ambayo wengi wanaitazama kama ya kujiingiza motoni.Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yameitaja Eritrea kama gereza moja kubwa sana ambayo huwatesa wafungwa.
Isaias Afewerki amekuwa Rais wa Eritrea tangu mwaka 1993
baada ya kupata uhuru kutoka kwa Ethiopia mwaka1993.
Madai haya yamekanushwa na serikali.
Vijana wa Eritrea lazima wajihusishe na shughuli za ujenzi wa taifa hadi wanapofika umri wa miaka 40 hali ambayo imesababisha takriban watu 3,000 kuitoroka nchi hiyo kila mwezi.
Katika barua yao, maaskofu hao waliandika kuwa watu wengi wanaitoroka nchi hiyo kwa hivyo watu wakongwe wa taifa kukosa watu wa kuwalea uzeeni.
Walisema kuwa wananchi wa Eritrea wanaelekea katika nchi salama, nchi ambazo zinawapa fursa ya kufanya kazi na ambako wana uhuru wa kujieleza pia nchi ambazo mtu anafanya kazi na kupata malipo.
Barua hiyo ilitiwa saini na maaskofu , Mengsteab Tesfamariam wa Asmara, Tomas Osman wa Barentu, Kidane Yeabio wa Keren na Feqremariam Hagos wa Segeneiti.
Makasisi hao wameitaka serikali kutowatesa wafungwa na pia kuwa na huruma na kisha kuwaruhusu kuwakilishwa mahakamani.
Baada ya kanisa la Orthodox, kanisa la kikatoliki ndilo la pili kwa ukubwa nchini Eritrea na wadadisi wanasema kwamba askofu mkuu wa Asmara,ana ushawishi mkubwa sana nchini humo.