Kiongozi wa kiislamu aliyeuwawa Kenya.
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/kiongozi-wa-kiislamu-aliyeuwawa-kenya.html
Kiongozi wa
wahubiri wa kiislam nchini Kenya ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji
wa mwambao wa Mombasa, yakiwa ni mauaji ya hivi karibuni.Sheikh Mohammed
Idris, mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa Kenya, ameuawa
karibu na msikiti uliopo karibu na nyumbani kwake na kundi la vijana
wenye silaha.Taatifa zinasema kuwa hapo awali amekuwa akipata vitisho
kutoka kwa baadhi vijana wa kiislam na kuhofia maisha yake.Waislam
kadhaa maarufu wenye msimamo mkali wamekua wakiuawa kwa kupigwa risasi
katika hali isiyoelezeka miaka ya hivi karibuni.
Wengine walikuwa wakituhumiwa kuwa ni viungo wa kundi la kiislam la
Al-Shabab la nchini Somalia ambapo wafuasi wao wamekua wakiishutumu
serikali kuhusika na mauaji hayo, shutuma ambazo mamlaka imezikataa.Hivi
karibuni Idris, alilitaka jeshi la polisi kupambana na vikundi vyenye
muelekeo wa kijeshi katika msikiti wake, na kupelekea wengine kumuona
kama msaliti.