Flatnews

Kiongozi ataka vijana wajihami Nigeria



Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa miaka mingi
Kiongozi mmoja wa kijamii katika mji wa Chibok Nchini Nigeria ameiomba serikali ya taifa hilo kuwaruhusu kubuni makundi ya vijana waliojihami ili kulinda vijiji vyao kutokana na makabiliano kutoka kwa kundi hatari la Boko Haram.
Pogo Bitrus ameiambia BBC kuwa hali ya kukata tamaa kutoka kwa raia wa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria inazidi kushuhudiwa kila uchao huku wengi wakihoji kuwa wanajeshi wa serikali wameshindwa kulinda raia.
Sasa wanasema njia pekee ya kukabiliana na uvamizi wa mara kwa mara ambapo mali na maisha yao yanapotea ni kuunda makundi ya kulinda vijiji.
Mnamo siku ya Jumanne, wanawake 20 walitekwa nyara na Boko Haram karibu na eneo ambako wasichana 200 walitekwa nyara mwezi Aprili.
Kiongozi huyo Dr Pogo Bitrus alisema kuwa kuna hasira kubwa miongoni mwa jamii kwamba serikali haifanyi juhudi za kutosha kulinda wananchi kutokana na mashambulizi ya kundi hilo.
Alisema watu wana haki ya kujihami ikiwa serikali haiwapi ulinzi.
Alisema mbinu zingine mbadala zinahitajika kukomesha visa vya wapiganaji hao kuteketeza na kuiba mali ya wananchi katika maeneo ambako Boko Haram wanatawala.
Silaha zaidi zinahitajika kupambana na wapiganaji hao ambao kiongozi huyo alisema wanaendesha vita via vya kidini Kaskazini mwa Nigeria.

Post a Comment

emo-but-icon

item