HII AMSHA AMSHA KWELI HATIMAYE SAKATA LA PICHA CHAFU ZA WEMA, DIAMOND ZATINGA BUNGENI
Sakata la mastaa wakiwemo Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kupiga picha chafu kisha kuzitundika mitandaoni limetinga bungeni baada y...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/hii-amsha-amsha-kweli-hatimaye-sakata.html
Mastaa Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakiwa kwenye pozi la kimahaba
Hilo liliibuka Suzi mjengoni katika kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Saidi Mtanda alitaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tabia za watu maarufu kupiga picha zisizo na maadili kisha kuziweka mtandaoni.
Katika kujibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema: “Tunajitahidi kuhakikisha wanaofanya hivyo wanachukuliwa hatua stahili ili kukabiliana na matendo hayo ambayo ni kinyume na maadili.”
Staa Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kwenye pozi lenye utata.
Katika
kuonesha kutoridhika na majibu ya waziri, Mheshimiwa Mtanda alipopewa
nafasi aulize swali la nyongeza alisema: “Mheshimwa spika nahisi swali
langu halijajibiwa ipasavyo. Nilichotaka kujua ni hatua ambazo
zimechukuliwa kwa baadhi ya watu mastaa kama vile Wema na Diamond ambao
hupiga picha zao zisizofaa kisha kuziweka mtandaoni.”Kufuatia swali hilo, Nkamia alisimama na kujibu kwamba, serikali imeweka mikakati na njia sahihi za kukabiliana na tabia hiyo na kwamba wale ambao watabainika watachukuliwa hatua zinazostahili.
Licha ya majibu hayo, bado wabunge walionesha kutoridhika, hali ambayo Spika Anne Makinda aliiona na yeye akaongezea “Waheshimiwa wanataka kujua na za hivi karibuni zilizovuja mtandaoni” ambapo jibu la Nkamia lilikuwa:
“Mheshimiwa kuhusu hizi picha za juzi zilizosambaa mtandaoni, tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua tutakapobaini zilikotokea.”