HAYA NDIO MAGARI YANAYOONGAZA KUVUNJA SHERIA
HUKU ajali za barabarani zikizidi kuongezeka kila siku hasa jijini Dar es Salaam, timu ya uchunguzi ya Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya ...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/haya-ndio-magari-yanayoongaza-kuvunja.html
HUKU ajali za barabarani zikizidi kuongezeka kila siku hasa jijini Dar es Salaam, timu ya uchunguzi ya Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, hivi karibuni lilifanikiwa kuyanasa baadhi ya magari kadhaa yanayokiuka sheria za usalama barabarani.
Magari hayo, ambayo yalikuwa kinara
wakati wa uchunguzi huo, yakiwemo yenye namba za usajili zinazoonyesha
kuwa ni kutoka idara mbalimbali za serikali, yalikutwa yakiendeshwa kwa
kasi maeneo yasiyoruhusiwa, yakitanua kinyume na utaratibu na wakati
mwingine yakipita katika makutano ya barabara, licha ya taa nyekundu
kuwaka.
Katika baadhi ya makutano ya barabara
kama vile Tazara, Bamaga na Ubungo, magari hayo, ambayo baadhi yao
yanaonekana katika ukurasa wa mwisho wa gazeti hili, yalipita kwa mwendo
kasi licha ya kuzuiwa na taa, hali ambayo inaleta uwezekano mkubwa wa
ajali.
OMF lilishuhudia gari lenye namba za
usajili T 896 BQQ baada ya kuvuka huku taa nyekundu zikiwaka,
almanusura limgonge mtembea kwa mguu aliyekuwa akivuka katika makutano
ya barabara ya Bamaga, Mwenge wilayani Kinondoni.
Gari
hilo lilitokea Mwenge likiwa katika mwendo wa kasi na halikujali kama
taa nyekundu zilikuwa zikiwaka (kuashiria lisipite) na magari mengine
yanayotokea Sinza kuelekea Sayansi yalikuwa yanapita.
Uchunguzi
umebaini kuwa vitendo hivi vya ukiukwaji wa sheria za usalama
barabarani hufanyika zaidi wakati askari wakiwa hawapo maeneo hayo,
lakini madereva hao huzingatia sana sheria endapo trafiki wakiwa eneo la
tukio.
OFM
inaendelea na kampeni ya kuyabaini magari yote yanayokwenda kinyume cha
sheria za usalama barabarani na kitayafikisha magari yote kwa Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga kwa hatua zaidi.
Aidha kwakuwa magari mengi ya daladala
pia yamo, OFM itayafikisha kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri
nchi kavu na majini (Sumatra) Ahmed Kilima.
GPL