https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/brazil-yaanza-kwa-kuitandika-croatia-3.html
Neymar Mkombozi: Mbrazil huyo anayevaa jezi namba 10 alifunga mawili.
NYOTA
aliyebeba matumaini ya Wabrazil wengi, Neymar amefunga mabao mawili
usiku huu katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Croatia kwenye mchezo wa
ufunguzi wa fainali za kombe la dunia.
Wenyeji
walijifunga mapema dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza baada ya Marcelo
kuujaza mpira nyavuni katika harakati za kuokoa na kuzua ukimya mkubwa
uwanjani kwa mashabiki wa Brazil waliofurika kushuhudia timu yao..
Mambo
almanusura yawe mabaya kwa Brazil wakati Neymar alipomfanyia faulo
mbaya kiungo wa Croatia Luka Modric, lakini mwamuzi Yuichi Nishimura
alimzawadia kadi ya njano tu.
Baadaye
Neymar alifunga bao la kusawazisha kwa shuti la mbali na aliongeza bao
la pili kwa njia ya mkwaju ya penati baada ya mwamuzi kutoa penati
yenye utata kufuatia Dehan Lovren kumfanyia madhambi Fred.
Oscar
alihitimisha karamu ya mabao kwa Wabrazil na kutoka na ushindi wa
kwanza katika michuano ya mwaka huu inayofanyika katika ardhi yao.
Mkwaju wa penati: Neymar alifunga penati yake ingawa kipa wa Croatia aligusa mpira.
Hapa chini ni viwango vya wachezaji wa timu zote na alama zimetolewa juu ya 10.
Neymar ndiye mchezaji bora wa mechi ya leo kwa kupata alama 8 akifuatiwa na Oscar mwenye alama 7.
Kikosi cha Brazil na viwango vyao: Julio
Cesar 6; Dani Alves 5.5, Thiago Silva 6, Luiz 6, Marcelo 5.5, Paulinho
6, Gustavo 7, Hulk 6 (Bernard 68), Oscar 7, Neymar 8, Fred 6.5.
Wachezaji wa akiba: Jefferson, Fernandinho, Dante, Maxwell, Henrique, Ramires, Hernanes, Willian, Jo, Maicon, Victor.
Kikosi cha Croatia na viwango vyao:
Pletikosa 6, Srna 6.5, Corluka 7, Lovren 6.5, Vrsaljko 6; Modric 7,
Rakitic 7, Perisic 6.5, Kovacic 6 (Brozovic 62), Olic 6, Jelavic 6.
Wachezaji wa akiba: Zelenika, Pranjic, Vukojevic, Schildenfeld, Rebic, Sammir, Vida, Eduardo, Subasic.
Anajiangusha chini kirahisi: Fred akianguka baada ya kupewa misukosuko na Dejan Lovren na mwamuzi aliwazadia penati Brazil
Luiz Felipe Scolari akimkumbatia Neymar baada ya kufunga bao la kusawazisha.
Neymar (kushoto)akishangilia bao lake la kwanza
Guu la kushoto: Neymar akipiga shuti nje ya eneo la hatari na kuutumbukiza mpira kwenye kona
Kipa wa Croatia Stipe Pletikosa akijaribu kuokoa shuti la Neymar lakini aliambulia manyoya tu
Bao la mbali kabisa: Goli la Neymar lilitoka nje ya boksi kama uonavyo kwenye picha ya juu.
Mshale huo unaonesha jinsi shuti la Neymar lilivyokuwa na nguzu na lililengwa eneo sahihi
Hakutarajia : Marcelo (wa pili kulia) alijifunga bao na kumwacha kipa Julio Cesar akiduwaa.