Flatnews

ASHA BARAKA- SITOMSAMEHE ALLY CHOKI

Posted by william Malecela on Wednesday, June 04, 2014



Mkurugenzi wa bendi ya African Stars aka Twanga Pepeta Asha Baraka, amesema kamwe hawezi kumsamehe mwanamuziki Ally Choki ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, ambaye ana bifu naye la muda mrefu.
 Hivi karibuni habari zilienea kuwa wawili hao wameshapatana baada ya kukutanishwa na chombo kimoja cha habari nchini, jambo ambalo Asha amelikanusha.

“Siwezi kupatana na Choki kwa sababu sioni haja ya kufanya hivyo. Nimesikia kwenye mitandao kuwa eti tumepatanishwa... watu bwana! Labda waliopatana ni wao siyo mimi. Nasisitiza habari hizo ni za uongo na ninaomba Choki akae mbali na mimi,” alisema Asha.

Post a Comment

emo-but-icon

item