WAZAZI KATAVI WAHIMIZWA KUKOMALIA UJENZI WA SHULE
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/wazazi-katavi-wahimizwa-kukomalia.html
Mwenyekiti wa Halamshauri ya Mji
wa Mpanda, Enock Gwambasa akizungumza na wazazi ( hawapo pichani) wa
Kata ya Mpanda hoteli katika kikao cha kujadili maendelo ya elimu na
ujenzi wa Shule hiyo.
Wazazi
wa wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari kashaulili wakimsikiliza
Diwani wao ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji katika kikao cha
kujadili maendelo ya ujenzi wa shule.
(Picha zote na Kibada Kibada )
Na Kibada Kibada-Mpanda Katavi.
Wazazi
katika Halmshauri ya Mji wa Mpanda Mkoani Katavi wamehimizwa kuwa
mstari wa mbele katika kujitolea kuchangia ujenzi wa shule ili wanafunzi
na walimu wao wapate mahali bora pa kusomea na kufundishia.
Rai hiyo
imetolewa na Mwenyekiti wa Halamshauri ya Mji wa Mpanda Enock
Gwambasa ambaye ni Diwani wa Kata ya Mpandahoteli wakati akiongea
katika kikao cha wazi cha kujadili maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na
wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya sekondari Kashaulili iliyoko
kata ya Mpandahoteli .
Pia
kikao hicho kilijadili kuongeza nguvu katika ujenzi wa vyumba vya
madarasa, maabara,nyumba za walimu na uzio wa shule ili shule iweze
kuwa katika mazingira mazuri ya ulinzi.
Ameeleza kuwa shule ni mali ya wazazi hivyo ni wajibu wa wazazi kuhakikisha wanajenga shule na kuilinda na kuitunza.
Akifafanua
zaidi Gwambasa alieleza kuwa yeye kama mlezi wa kata anasimamia
shughuli zote za maendeleo ya Kata ikiwemo sekta ya elimu .
Pia
ni wajibu wake kusimamia shughuli nyingine za maendeleo katika
halmashauri ya mji wote kwa kuwa yeye ndiye mwenye dhamana hiyo na
amekutana na wazazi wa Mpanda Hoteli ili kupanga mipango ya maendeleo ya
shule hususani kuboresha elimu katika Kata na Halamsahauri kwa ujumla.
Kuhusu
taalamu amewahimiza walimu na wanafunzi kuchapa kazi kwa bidii ili
kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kwa kuwa shule hiyo imekuwa na historia mbaya ya kutokufanya viziru katika mitihani wa kidato cha nne .
Awali
Mkuu wa Shule ya Sekondari kashaulili, G Nyaronga alieleza kuwa Shule
yake inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa na jengo la
utawala hali inayowafanya walimu kutumia darasa kama jengo la utawala na
hivyo kuongeza upungufu zaidi wa madarasa katika shule hiyo.
Mkuu
huyo wa shule alieleza kuwa madarasa yaliyopo ni 14 tu kwa ajili ya
wanafunzi 654 na vyumba hivyo havitoshi, hivyo ipo haja ya kuona wazazi
wanafanya jitihada kujenga vyumba vingine zaidi.
Mbali
ya ujenzi wa madarasa pia wanahitaji kujenga vyumba viwili vya
maabara,ukamilishaji wa majengo yaliyoanza kujengwa ,hivyo upatikanaji
wa matofali ni muhimu sana ili kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kwa
wakati na hilo ni kazi ya wazazi kwa kushirikiana na uongozi wa shule na
serikali kwa ujumla.