Flatnews

WASTARA NA BOND MAMBO YAWEKWA HADHARANI

ANATOKA KIMAPENZI NA WASTARA?



ANATOKA KIMAPENZI NA WASTARA?
Nakukubali sana kaka Bond lakini napenda kukuuliza kwamba kuna madai kuwa unatoka kimapenzi na Wastara Juma (mwigizaji). Je, ni kweli? Husna, 0689341478.
BOND: Siyo kweli. Mimi ni meneja wa Wastara. Pia ni mwongozaji wake wa filamu kwa hiyo tuna mikataba mingi ya kufanya kazi muda mrefu sana.
UHUSIANO NA AUNTY LULU
Kiukweli kama una uhusiano na Aunty Lulu (Semagongo) mwache tu kwa sababu hutamuweza, skendo zake zinatisha lakini mimi nakushauri  usimuache hivihivi, mshauri vizuri, awe mwelewa kwani anatakiwa kuwa na msimamo mzuri. Msomaji, 0764158569.
BOND: Asante, Aunty Lulu nilishaachana naye muda mrefu lakini huwa naendelea kumshauri vitu vingi kwa hiyo yeye ndiye anayeamua kuchukua ushauri au kuacha.
OA SASA
Kuwa na uhusiano ni sawa kwani umri unakata mbuga, kwa maoni yangu uoe sasa. Msomaji, 0785606175.
BOND: Asante nitalifanyia kazi hilo, namuomba Mungu anijalie.
USHAURI
Mimi napenda kuigiza na kipaji ninacho lakini bado mchanga kisanaa ila natamani kutimiza ndoto yangu nifanyeje? Naomba nisaidie. James Salamba, 0768558834.
BOND: Ongea vizuri na wazazi wako kwa sababu siku hizi kuna shule nyingi zinazofundisha sanaa ujiunge nazo au uende kwenye vikundi vya sanaa, naamini utatimiza ndoto yako.
FILAMU NGAPI? ANA MCHUMBA?
Mpaka sasa una filamu ngapi na je, una mchumba? Msomaji, Mwanza, 0765757273.
BOND: Nina filamu saba mpaka sasa na nina mchumba.
UTULIVU
Nakukubali sana kaka ila naomba utulie. Mariam Said, Gairo, 0656977555.
BOND: Asante sana na mimi siku zote nimetulia huwa sihangaiki.
ALISHAKUWA TEJA?
Nasikia ulishawahi kuwa teja, ni kweli? Frank, Mwanza, 0752157695.
BOND: Sijawahi na ninamuomba Mungu aninusuru.
AUNTY LULU TENA
Kwa ushauri wangu achana na umsahau kabisa huyo Aunty Lulu. Specioza, Mwanza, 076507479.
BOND: Asante ila kwa pamoja ninaomba tumuombee Aunty Lulu abadilike pia tuendelee kumshauri.
ILIKUWAJE?
Ilikuwaje mpaka ukaachana na Aunty Lulu maana mlikuwa mnapendana sana? Salumu Kabunda, Iringa, 0763236597.
BOND: Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho, naona mwisho wetu ulikuwa wa hapahapa duniani.
WALIMWAGANA KITAMBO
Vipi kaka bado mnaendelea na uhusiano wa kimapenzi na Lulu Semagongo au mmeshamwagana? Zamrata Makame, Dar, 0688909490.
BOND: Tulishamwagana siku nyingi.
NAOMBA AWE MCHUMBA WANGU
Bond namkubali kwenye mambo yake na kwa vile hajaoa naomba achukue namba yangu, nahitaji awe mume wangu. Ashura, Mtwara, 0712231020.
BOND: Nashukuru na nimefurahi kwa kunikubali ila nina mchumba tayari, nakuombea kwa Mungu akupatie mume mwema.
GPL

Post a Comment

emo-but-icon

item