WANACHAMA SIMBA SC OGOPENI `SIASA NYEPESI` MITHIRI YA UKOMA WAKATI HUU WA UCHAGUZI, KUMBUKENI HAYA….
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/wanachama-simba-sc-ogopeni-siasa.html
WANACHAMA
wa Simba sc kuna mambo mengi yanayoendelea kuelekea uchaguzi mkuu wa
klabu yenu utakaofanyika juni 29 mwaka huu, hasa baada ya mgombea mmoja
wa Urais, Michael Richard Wambura kuenguliwa kutokana na sababu tofauti.
Kuenguliwa
kwa Wambura na kamati ya uchaguzi wa Simba chini ya mwenyekiti wake,
mwanasheria na wakala wa wawachezaji wa FIFA, Dkt. Damas Ndumbaro
kunaonekana kuvuta hisia za wadau wengi wa soka na wanachama wa Simba
wenye mapenzi makubwa kwa mgombea huyu.
Ni
dhahiri wapo wanachama wengi wenye mapenzi makubwa kwa Wambura na piga
ua galagaza wao wanajua kiongozi anayeifaa Simba kwa sasa ni huyo.
Lakini
kumbuka pia kuwa wagombea wengine, Evans Aveva na Andrew Tupa. Wote
hawa wanaungwa na watu wengi nyuma yao. Lakini yawezekana sababu
zikatofautiana.
Aveva
ana wapenzi wengi wanaohitaji kumuona katika kiti cha Urais wa Simba
kuanzia juni 29 mwaka huu. Ni dhahiri kuwa Aveva ni moja ya wagombea
wenye nguvu kwenye uchaguzi huu.
Ushahidi
wa mamia ya mashabiki waliomsindikiza kuchukua fomu na kurudisha fomu
unatosha kuamini kuwa Aveva anaungwa mkono na wanachama wengi, ingawa
bado si rahisi kujiridhisha kuwa wote wale ni wanachama halali wa Simba.