Jaguar alitaka atumiwe ticket ya ndege
ya business class, alitaka achukuliwe chumba kwenye hoteli ya nyota
tano, apewe ulinzi popote atakapokwenda na vilevile apewe gari zuri la
kifahari la kutembelea.
Kwenye sharti jingine Jaguar alitoa
option kwa waandaaji na kuwaambia kama wangeshindwa kumpa ticket ya
ndege basi walipaswa kuweka mafuta ili aje na ndege yake ndogo
anayomiliki.
Chameleone, Wyre, Amani, Ay, Mtangazaji
William Tuva, shabiki Daudi wa Kota na Dj wa Chameleone juzi Dar es
salaam.Alipohojiwa na ghafla.co.ke Jaguar alisema asingeweza kuhudhuria
tukio ambalo asingepewa heshima aliyoitaka kama ambavyo huwa anaipata
anapokwenda kwenye nchi nyingine katika matukio kama haya ndio maana
ilikua bora ahudhurie harusi na kuongeza kwamba ‘nitahudhuria iwapo
wataanza kuwa-treat vizuri wasanii wa Kenya’
Tuzo za KILI 2014 zilihudhuriwa na
mastaa wawili wa Kenya ambao ni Wyre na Amani huku Uganda ikiwakilishwa
na Jose Chameleone ambae ndio alitangazwa mshindi kwenye kipengele cha
Afrika Mashariki.