AIBU KWA TAIFA JIONEE BAADHI YA WANAFUNZI WA SEKONDAR WALIVYO KWENYE MAPOZ YA KUJIUZA MKOANI TANGA..NOUMASANA.
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/aibu-kwa-taifa-jionee-baadhi-ya.html
BAADHI
ya wakazi wa jijini Tanga, wameomba uongozi wa Wilaya ya Tanga kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi, kuweka mkakati endelevu, utakaodhibiti
wimbi la vijana wa kike wanaojiuza miili yao nyakati za usiku kwenye
baadhi ya barabara za katikati ya mji na bustani za kupumzikia.
Wamesema
hatua hiyo, itasaidia kukomesha vitendo hivyo vinavyoendelezwa bila
woga na kudhibiti kasi ya ongezeko lao, hasa katika barabara ya
Independence na Bustani ya Forodhani nyakati za jioni.
Aisha
Zahoro, mkazi wa Chumbageni alisema hali ni mbaya zaidi katika Bustani
ya Forodhani, ambapo wasichana wadogo hasa wale wenye umri wa kusoma
shule za sekondari, wamefikia hatua ya kuvua nguo zao ili kuonesha wazi
maumbile yao kwa baadhi ya wanaume, wanaofika eneo hilo kwa lengo la
kuwachukua.
“Sikuamini
macho yangu usiku wa saa 2 hivi, nikiwa hapo bustanini nimeketi kwenye
viti vilivyoko karibu na miembe mikubwa, pembeni walisimama wasichana
kadhaa nikadhani nao wamekuja kupunga upepo au kupata vyakula hapo.
Lakini kumbe sivyo, wenzangu hao walikuwa kazini…nilishangaa kwani
walipofika wanaume wawili, wenzangu walianza kuzungumza nao biashara,
ghafla mmoja kati yao akafunua nguo alizokuwa amevaa, akitamba kwamba
‘nitazame mimi sina kovu hata moja mwilini,” alisema.
Alisema
wasichana hao wanajiuza kwa bei za kati ya Sh 2,000 kwa huduma ya
haraka (chapchap) hapo hapo bustanini, Sh 5,000 kinyume na maumbile na
Sh 10,000 ndani ya gari la mteja.
Alidai kwamba vitendo hivyo, sasa vimevuta wasichana wengi wadogo, ambao walipaswa kuzingatia masomo.
Hassan
Sadoki alisema ili kusaidia kudhibiti hali hiyo, ambayo sasa inaleta
sifa mbaya ndani ya Jiji ni vema ufanywe msako endelevu wa kuwakamata na
kuwaadhibu ili iwe mfano kwa wengine, wanaotaka kuendeleza vitendo
hivyo, kwa lengo la kujipatia fedha ya kujikimu kimaisha.
Kwa
upande wake, Audax Msofe, mkazi wa Namiani, alisema binafsi anaamini
vijana wanaofanya biashara ya ngono katika mitaa mbalimbali ya jijini
humo, ikiwemo kwenye bustani, wanahitaji kujengwa kwa maadili ya kidini
ili wawe na hofu ya Mungu.
“Naamini
msako wa polisi peke yake hautatosha kuwadhibiti, badala yake viongozi
wa dini nao washirikishwe katika suala hili kwa kuendelea kuzungumza na
waumini wao hasa vijana, ambao hivi sasa wanaonekana hawana kabisa hofu
ya Mungu mioyoni mwao na hivyo kuamua kujiingiza kwenye vitendo viovu”,
alisema.