UBALOZI WA TANZANIA KATIKA UAE WASHEREHEKEA SHEREHE ZA MIAKA 50 MUUNGANO WA TANZANIA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/ubalozi-wa-tanzania-katika-uae.html

Balozi wa
Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu,Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk
(kushoto) akimpokea mgeni rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya
Muungano Tanzania, Mheshimiwa Dr. Hadef Jawa’n Al Dhaheri, Waziri wa
Sheria wa UAE,katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya
Intercontinental,Abu Dhabi..
Balozi
Mbarouk akimuongoza Mgeni rasmi Mhe. Dr. Hadef Jawa’n Al Dhaheri,
Waziri wa Sheria wa Umoja wa Falme za Kiarabu, pamoja na Mabalozi wanao
wakilisha nchi zao hapa UAE kuingia katika ukumbi wa Sherehe.
Mhe.
Balozi, Mgeni Rasmi na baadhi ya Mabalozi wanao wakilisha nchi zao
nchini UAE, wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa za UAE na Tanzania.
Balozi Mbarouk akitoa hotuba katika sherehe hizo.
Baadhi ya wageni waalikwa, akiwepo Mhe. Mallallah Mubarak (mwenye kilemba cheupe), aliyewahi kuwa Balozi wa UAE nchini Tanzania.
Balozi
Mdogo wa Ubalozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Bw. Omary Mjenga akiwa na
familia yake na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi.
Wageni waalikwa wakipata chakula.
Balozi
Mbarouk akiwa na wachezaji mashuhuri wa zamani wa timu za Yanga, simba
na Timu ya Taifa, Alluu Ally, Omar Hussein na Yanga Bwanga wanaoishi
nchini UAE.
Watanzania wanaoishi nchini UAE.
Balozi Mbarouk akiwa na Watanzania wanaoishi UAE.
Balozi Mbarouk akiwa na viongozi wa Chama cha Watanzania wanaoishi UAE.
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi
Mdogo Bw. Omary Mjenga akiwa pamoja Mwenyekiti wa Watanzania nchini UAE
Bw. Mohammed Sharif na wageni waalikwa.










