Flatnews

KINANA AFUTA NYAYO ZA UKAWA ZANZIBAR




Wananchi wakishangilia na kuonesha vidole kuunga mkono serikali mbili za Muungano wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM leo kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.Mkutano huo uliudhuriwa na viongozi mbalimbali  akiwemo Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana
Mama Fatma Karume akihutubia katika mkutano huo na kukemea Ukawa wanaotaka kuuvunja Muungano kwa kutaka Serikali Tatu katika mabadiliko ya Katiba mpya.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhman Kinana akimpongeza Mjane wa Hayati Abeid Amani Karume, kwa hotuba yake nzuri katika mkutano huo.


Wananchi wakishangilia katika mkutano huo hasa baada ya Mjumbe wa NEC, Mohamed Seif Khatib kumuelezea Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kuwa na tabia ya kinyonga  kuhusu suala la Muungano, ambapo awali alikuwa muuminji Muungano wa Serikali tatu, mara wa mkataba na sasa anataka Serikali tau


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Balozi Ali Seif Idd akihutubia katika mkutano huo na kupendekeza UKAWA kufutwa kwa vile haina uhalali wowote akidai kuwa si chama kwani haina usajili. Alisema kuwa Ukawa imeundwa kwa lengo la kuuvunja Muungano uliodumu kwa miaka 50 na kudumisha amani na umoja kwa Tanzania.
Kinana na viongozi wengine wakiuombea dua muungano wa Tanzania pamoja viongozi waanzilishi wa muungano huo ambao ni Julius Nyerere na Abeid Karume.
Mjumbe wa Bunge la Katiba,Asha Bakari Makame akimchana chana Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kwa tabia yake ya kinyonga kuhusu muundo wa Muungano.

Post a Comment

emo-but-icon

item