TAIFA STARS YAWASILI MBEYA KULA KIPUPWE CHA TUKUYU KUWAWINDA ZIMBABWE
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/taifa-stars-yawasili-mbeya-kula-kipupwe.html
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars imewasili
Mjini Tukuyu jijini Mbeya tayari kwa kuweka kambi ya kujiwinda na mchezo wa
marudiano dhidi ya Zimbabwe mjini Harare kuwania kupangwa katua ya makundi ili
kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON mwakani
nchini Morocco.
Stars imeamua kuweka kambi Mbeya kutokana na hali
ya hali ya baridi iliyopo mkoni huko kwani inafanana na hali ya hewa ya Zimbabwe.
Katika mechi ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam juni 18 mwaka huu, Taifa stars iliibuka na ushindi wa mbao
1-0.
Bao hilo pekee lilifungwa na mshambuliaji wa kati
wa Stars, John Raphael Bocco `Adebayor`.
Stars inahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili
kusonga hatua inayofuata.
Kocha mkuu wa Stars, Mart Nooij baada ya kuwasili
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songweni jijini humo, alisema anaamini Tukuyu
ni eneo tulivu sana, hivyo vijana wake watajiandaa vizuri.
Nooij alisema ana matumaini makubwa ya kusonga
mbele katika mchezo wa marudiano ingawa anakiri wazi kuwa mechi hiyo itakuwa na
ushindani mkubwa.
Mholanzi huyo aliongeza kuwa anaenda kuyafanyia
marekebisho makosa ya safu ya ushambuliaji
na nafasi ya kiungo ambayo ilionekana kupwaya sana.
Mchezo uliopita, sehemu ya beki ya kulia
iliyoongozwa na Shomary Kapombe na kushoto, Oscar Joshua ilionekana kuwa na
matatizo, ingawa kipindi cha pili wachezaji hawa walibadilika.
Mwinyi Kazimoto na Frank Domayo walishindwa kuwa
na uelewano katika safu ya kiungo na kuwaruhusu Wazimbabwe kucheza sana mpira.