SNURA AFUNGUKA KUHUSU DIAMOND
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi amefunguka kwamba tuzo saba za Kilimanjaro alizopata msanii mwenzake, Nasibu Abdul al...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/snura-afunguka-kuhusu-diamond.html
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Snura
Mushi amefunguka kwamba tuzo saba za Kilimanjaro alizopata msanii
mwenzake, Nasibu Abdul alistahili kuzipata kwani anajituma.
Msanii wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi, 'Mama Majanga'.
Akichonga na gazeti hili, Snura alisema
Diamond ni mwanamuziki anayejituma sana pia ni mbunifu na juhudi zake
ndizo zimemfanya ashinde tuzo zote hizo.
“Mimi nilikuwa kwenye kipengele cha
msanii chipukizi lakini haikuwa bahati yangu, naamini wakati wangu
ukifika nitapata tuzo sina haraka ila kwa shemeji Diamond alistahili
kupata,” alisema Snura.
GPL