PELLEGRINI: KITU KIBAYA ZAIDI WATAKACHOFANYA WACHEZAJI WA MAN CITY NI KUWAZA TAYARI WAMECHUKUA TAJI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/pellegrini-kitu-kibaya-zaidi.html?m=0
Ushindi
wa jana uliwafanya City wakalie usukani wa ligi hiyo kwa wastani mzuri
wa mabao dhidi ya Liverpool, huku wakisaliwa na mechi mbili kumaliza
msimu.
Man
City wanaweza kutwaa ubingwa kama watashinda mechi zote mbili za mwisho
dhidi ya Aston Villa na West Ham, lakini Pellegrini amesema mbio za
ubingwa hazijakamilika bado.
“Nadhani
kitu kibaya zaidi tutakachokifanya ni kuanza kuwaza kuwa tumemaliza
mbio za ubingwa sasa”. Pellegrini amewaambia waandishi wa habari.
“Tutakutana
na timu ambazo hazina presha, lakini ni michezo muhimu sana. Kuanzia
kesho (leo) tunaanza kuifikiria mechi ijayo dhidi ya Aston Villa-kila
mchezo tunauchukulia uzito wa hali ya juu”.
“Nadhani
ni muhimu kuendelea kufanya vizuri kama tufanyavyo sasa-mechi na
Everton ilikuwa ya mwisho ugenini na tulianza msimu huu kwa kuvuna
pointi nne kwa mechi sita za kwanza ugenini, kwa mazingira haya nadhani
timu inafanya vizuri”.
Mabao
mawili ya Edin Dzeko na moja la Sergio Aguero liliwapa ushinda Man City
dhidi ya Everton, lakini Pellegirini amekiri kuwa ulikuwa mchezo mgumu
kwa timu yake.
“Everton
walicheza mpira mzuri toka mwanzo, unaweza kuona kuwa walitaka kushinda
tangu mwanzoni mwa mchezo, hakika ulikuwa mchezo mgumu sana kwetu”.